Suzanna Owiyo anaomboleza

Mwanamuziki Suzanna Owiyo amefiwa na babake mzazi na yeye ndiye alijukikanisha hayo kupitia Twitter. Mwimbaji huyo wa mtindo wa Benga aliweka picha kadhaa za marehemu babake na kuandika, “Ni vigumu kukuaga. Najua uko mahali pazuri, ambapo hakuna maumivu. Una amani sasa. Utaishi moyoni mwangu milele. Asante kwa kuwa baba mzuri na mwelekezi kwa wengi. Lala salama baba. Hadi tutakapokutana tena.”

Also Read
King Kaka Asema Ameugua Kwa Muda

Suzanna ambaye aliimba wimbo Kisumu 100, pia alibadilisha picha ya utambulisho kwenye akaunti yake ya Twitter akaweka ile ya mshumaa ambayo hutumika sana kuashiria maombolezi.

Wafuasi wake wengi kwenye twittwer na hata wasanii wenza walimwandikia maneno ya kumtia moyo Suzanna wakati huu mgumu.

Mwanamuziki King Kaka anayejiita @RabbitTheKing kwenye twittwer aliandika, “Ninakuombea. Naomba wewe na watu wako wa karibu mpate amani.”

Also Read
Juliani na chama cha Jubilee wazozania hakimiliki

Aliyekuwa jaji mkuu Dr Willy Mutunga aliandika, “Pole Sana. Sote tunatoka kwa Allah. Kwa Allah hakika tunarudi.”
Joyce Lay mwakilishi wa zamani wa kina mama katika kaunti ya Taita Taveta aliandika, “Pokea rambirambi zangu Suzanna kwa kufiwa na babako. Mwenyezi Mungu na akupe nguvu na aufariji moyo wako anapoilaza roho yake kwa amani.”

Also Read
Safari za ndege Kati ya Nairobi na Mombasa kusitishwa tarehe 29 mwezi huu

Terry Chocolat ambaye ni rafiki ya mwanamuziki Suzanna Owiyo alimwomboleza marehemu Owiyo akisema kwamba ameiaga dunia wiki tatu tu baada yake kumzuru nyumbani kwake huko Kasae.

Anaongeza kusema kwamba wazazi wa rafiki zake huwa wa maana kwake kwa njia sawia.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi