Taasisi ya KMTC kujengwa katika eneo bunge la Ndhiwa

Hazina ya maendeleo ya eneo bunge la Ndhiwa imetenga shilingo milioni 28 kwa ujenzi wa taasisi ya kutoa mafunzo ya utabibu (KMTC), Ndhiwa mjini.

Kwa mujibu wa mbunge wa eneo hilo Martin Owino, huo utahakikisha wanaokamilisha masomo katika eneo hilo wanapata mafunzo ya utabibu yatakayowawezesha kuajiriwa katika sekta ya afya.

Also Read
Marekani yahimizwa kuondoa agizo la kuzuia raia wake kuzuru Kenya

Akizungumza Jumatano wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa taasisi hiyo,Owino alisema taasisi hiyo itakuwa kielelezo cha masomo ya juu katika eneo buge hilo.

“Taasisi hiyo itaaanza kwa kutoka masomo ya kuweka rekodi za hospitali, mafunzo ya huduma ya afya ya jamii na masomo mengine ya vyeti na stashahada, “ alisema Owino.

Also Read
Wizara ya Afya yathibitisha visa 1,530 zaidi vya maambukizi ya COVID-19

Mbunge huyo alielezea matumaini kuwa taasisi hiyo itaboresha uchumi katika eneo bunge hilo.

“Wahudumu wa boda boda, mama mboga na pia wenye nyumba watafaidika pakubwa na taasisi hiyo. Nawasihi wenye nyumba kuanza kujenga nyumba zaidi za kukodisha wanafunzi,” alisema Owino.

Also Read
Jamii ya Maasai yasema inaunga mkono ripoti ya BBI

Owino alitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Homa Bay kutoa ekari tatu zaidi za ardhi kwa taasisi hiyo akisema taasisi hiyo ina ekari tano pekee ambazo hazitoshi.

 

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi