Taasisi ya Mitaala, KICD, yakamilisha uchapishaji vitabu vya Gredi ya 5

Taasisi ya kustawisha mtalaa wa masomo humu nchini, KICD, inakamilisha uchapishaji mtalaa wa masomo kwa wanafunzi wa gredi ya 5 ili kuzuia kucheleweshwa usambazaji vitabu kwa mwaka ujao wa masomo.

Taasisi ya KICD inasema utayarishaji vitabu vya masomo na vile vya kutoa mwongozo kwa waalimu wa gredi ya 5 umekamilishwa.

Hatua hii itahakikisha wachapishaji wanapata muda wa kutosha wa kuchapisha vitabu vya kiada kwa wanafunzi ambao kwa sasa wako gredi ya 4 wanaojiunga na gredi ya 5 katika mwaka ujao wa masomo.

Also Read
Madaktari kuanza mgomo wao Jumatatu huku wauguzi nao wakidinda kurejea kazini

Kwenye taarifa, taasisi ya KICD imesema utayarishaji mtalaa wa masomo kwa wanafunzi wa gredi ya 6 unafanyiwa utathmini wa mwisho.

Taasisi hiyo kwa sasa iko kwenye harakati ya kutayarisha mitalaa wa masomo kwa wanafunzi ya gredi za 7 hadi 9 na pia inajiandaa kutayarisha mitalaa ya masomo kwa wanafunzi wa gredi za 10 hadi 12.

Also Read
Wahudumu wa bodaboda waonywa dhidi ya ukiukaji wa sheria

Haya yamefichuliwa wakati wa kikao cha siku tatu cha Kamati ya Taasisi ya KICD ya kutoa uhamasisho na ushauri kwa waalimu kuhusu masuala ya mitalaa ya masomo.

Akiongea wakati wa kuhitimisha kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Elimu, Elyas Abdi, amewataka wanachama wa kamati hiyo kuhakikisha wanazingatia lengo la kuwa na mtalaa wa masomo wenye uadilifu katika kukuza talanta za wanafunzi.

Also Read
Jengo la kanisa la JCC Kisumu labomolewa

Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Taasisi ya KICD Profesa Charles Ong’ondo amehimiza kamati hiyo kuhakikisha inajizatiti vilivyo katika kuratibu mitalaa na vifaa bora vya masomo.

  

Latest posts

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

Shule 43,000 kote nchini kuunganishiwa mtandao wa internet

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi