Taasisi za Elimu Kufunguliwa Alhamisi na Sio Jumatatu

Wizara ya elimu imetangaza tarehe mpya ya kufunguliwa kwa taasisi za elimu kote nchini ambayo ni Alhamisi tarehe 18 mwezi huu wa Agosti mwaka 2022. Taasisi hizo ambazo nyingi hutumika kama vituo vya kupigia kura zilifungwa ghafla kabla ya uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi Agosti. Waziri wa elimu Profesa George Magoha wakati wa kutangaza kufungwa kwa taasisi hizo alielekeza kwamba zifunguliwe baada ya uchaguzi huo tarehe 11 jambo ambalo alionelea halingewezekana kutokana na shughuli nzima ua kujumlisha kura na kutangaza washindi.

Also Read
Shule za Msingi na Upili za umma kupokea madawati zaidi
Also Read
Vituo Vingi Vya Kupigia Kura Vyafungwa

Magoha alitoa taarifa ambayo ilielekeza kwamba wazazi wakae na wanao nyumbani hadi tarehe 15 ndio warejee shuleni. Kutokana na mpangilio wa pole pole wa kujumlisha na kutangaza kura za wadhifa wa urais, wizara ya elimu nchini Kenya imeahirisha ufunguzi wa taasisi hizo za elimu.

  

Latest posts

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi