Tahadhari yatolewa huku nchi hii ikitarajia mvua kubwa

Watu wanao-ishi katika maeneo ambayo hukumbwa mara kwa mara na maporomoko ya ardhi wameshauriwa wawe waangalifu huku nchi hii ikitarajia ongezeko la mvua wiki hii.

Taarifa ya idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini, inasema mvua kubwa za zaidi ya mm-20 katika muda wa masaa 24 zinatarajiwa kwenye kaunti za Magharibi na kati kati mwa Kenya siku ya Ijumaa wiki hii.

Also Read
Idadi ya watalii wanaozuru mbuga ya Hells gate yaongezeka

Mvua hizo huenda zikaongezeka hadi mm-30 katika maeneo ya magharibi mwa nchi siku za Jumamosi na Jumapili lakini zitapungua siku ya Jumatatu.

Also Read
Polisi wampiga risasi na kumuua mtu mmoja kwa kutovalia barakoa Malaba

Maeneo hayo ni kama vile kaunti za Uasin Gishu, Nandi, Trans Nzoia, Vihiga, Bungoma, Kakamega, Elgeyo Marakwet, Narok, Bomet, Kericho, Nakuru, Migori, Nyamira, Kisii, HomaBay, Kisumu, na Siaya.

Aidha huenda kukawa na hali kama hiyo kwenye kaunti za Busia, Pokot Magharibi, Turkana, Samburu, Baringo, Nyeri, Kiambu, Laikipia, Nyandarua, Murang’a, Embu, Meru, Kirinyaga, na Tharaka Nithi.

Also Read
Mwezi Februari utakuwa wa kiangazi – Utabiri

Kulingana na ushauri wa wataalamu wa utabiri wa hali ya hewa, wakaazi wa maeneo hayo wanapaswa kuwa waangalifu kuhusu uwezekano wa kutokea mafuriko.

  

Latest posts

#KisaChangu: Dr Mukhisa Kituyi kuwania urais ili kukamilisha safari ya ukombozi

John Madanji

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi