Taharuki yatanda Mandera kufuatia mauaji ya mchungaji mmoja wa mifugo

Taharuki imetanda kwenye kaunti ya Mandera kufuatia mauaji ya mchungaji mmoja wa mifugo katika sehemu ya Alungu,kaunti ndogo ya Lafey.

Viongozi wa sehemu hiyo wamekashifu vikali mauaji hayo.

Wakiongozwa na gavana wa Mandera Ali Roba,viongozi hao walitoa wito kwa wakazi wa sehemu hiyo kuwa watulivu na kutoa fursa kwa maafisa wa usalama kuchunguza kisa hicho.

Also Read
Familia 2000 zajisajili kwa bima NHIF

Viongozi hao walihimiza maafisa wa usalama kuharakisha uchunguzi huo na kuwachukulia hatua waliohusika katika juhudi za kutuliza hamaki ya wakazi wa sehemu hiyo.

Also Read
Uchunguzi umeanzishwa kuhusu mauaji ya simba huko Mara

Roba alisema matokeo ya mapema ya uchunguzi huo yamebaini kwamba huenda mauaji hayo yalitekelezwa na wahalifu.

Aliwasihi wakazi wa sehemu hiyo kutojihusisha kamwe na visa vyovyote vya ulipizaji kisasi.

Also Read
Kenya na Uganda zaafikiana kuondoa vikwazo vya kibiashara

Kiongozi wa waliowengi kwenye bunge la kaunti ya Mandera Abdi Ali, alitoa wito kwa serikali kuwachulia hatua wanaoeneza chuki kwenye mitandao ya kijamii,akisema kuwa wanaweza kuchochea ghasia endapo hawatachukuliwa hatua mwafaka.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi