Taharuki yatanda Samburu Kaskazini kufuatia kisa cha wizi wa mifugo

Hali ya taharuki imetanda Samburu Kaskazini kufuatia kisa cha wizi wa mifugo ambapo wachungaji wawili wa mifugo waliuawa kwa kupigwa risasi na zaidi ya ng’ombe 300 kuibwa katika eneo la Marti.

Akithibitisha kisa hicho kamishna wa kaunti wa Samburu Abdirisack Jaldesa aliwahakikishia wafugaji kuwa serikali ya kitaifa imezindua juhudi za kuhakikisha ng’ombe hao walioibwa wanapatikana na kurejeshewa wenyewe ili kuzuia visa vya ulipishaji kisasi.

“Kama kamati ya usalama tunataka kuhakikisha kuwa ng’ombe hao walioibwa siku ya Jumatatu na mbuzi walioibwa siku iliyotangulia wanapatikana,” alisema Jaldesa.

Also Read
Watumishi wa umma wahimizwa kujitokeza kuchanjwa dhidi ya Covid-19

Gavana wa kaunti ya Samburu Moses Lenolkulal, mbunge wa Samburu kaskazini Alois Lentoimaga, mwakilishi wanawake Maison Leshoomo, Seneta wa Samburu Steve Lelegwe na mbunge wa Samburu Mashariki Jackson Lekumontare miongoni mwa viongozi wengine walitembelea familia zilizoathirika na kisa hicho katika eneo la Marti.

Viongozi hao walitoa wito kwa wafugaji hao kuishi kwa amani na kusubiri serikali iwatafute mifugo hao.

Also Read
Serikali yapewa siku kumi kutatua uraia wa balozi Mwende Mwinzi

“Tumeachia serikali ya kitaifa jukumu la kuwatafuta mifugo hao huku tukiwahimiza wafugaji kuishi kwa amani,” alisema mwakilishi wanawake wa Samburu Maison Leshoomo.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Samburu Moses Lenolkulal, alitoa wito kwa serikali kuhakikisha familia za wachungaji mifugo wawili waliouawa na wezi hao wa mifugo, zinapata haki huku majina ya washukiwa yakikabidhiwa maafisa wa polisi.

Mbunge wa Samburu kaskazini Alois Lentoimaga aliwalaumu maafisa wa polisi kwa kuzembea kuzuia visa vya wizi wa mifugo na kushindwa kuwapata mifugo walioibwa katika eneo hilo.

Also Read
Wafugaji wahimizwa kutumia mbinu za kisasa za ufugaji

“Polisi wa eneo hili wameshindwa kudumisha sheria kuhakikisha amani na utangamano, mifugo wanaibwa na kwa maafisa hao inakuwa ni jambo la kawaida,’ alifoka Lentoimaga.

Miili ya wachungaji hao wawili wa mifugo ilipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya rufaa ya kaunti ya Samburu mjini Maralal.

  

Latest posts

Aden Duale: Uchaguzi Mkuu sharti uandaliwe tarehe 9 mwezi Agosti mwaka 2022

Tom Mathinji

Mudavadi asema taifa hili halipaswi kushuhudia ghasia kama zile za mwaka 2007

Tom Mathinji

Malkia Strikers wajizatiti lakini waanguka seti 3-0 mikononi mwa wenyeji Japan

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi