Tanasha Donna tena!

Kupitia kwa Edgar Obare ambaye amebandikwa jina la “The Tea Master” kwa kufichua mambo, mkenya mmoja amelalamika kwamba mwanamuziki Tanasha Donna aliwatapeli.

Mkenya huyo anadai kwamba walikwenda kwenye sehemu moja ya burudani huko Diani ambapo walilipa ada ya kuingia shilingi 500 kwa ajili ya kutumbuizwa na Tanasha.

Kulingana naye wateja walisubiri bila mafanikio kufurahikia tumbuizo la Tanasha ndio baadaye wakaarifiwa kwamba mwanamuziki huyo hangeweza kuwaimbia lakini wangeweza kupiga naye picha.

Also Read
Shilole afurahia ufuasi mkubwa Instagram

Mteja huyo anasema mmiliki wa sehemu hiyo ya burudani alilazimika kuwapoza wateja kwa kuwapa vinywaji bila malipo.

Lakini baadaye hapo hapo kwenye akaunti ya Instagram ya Edgar Obare ilieleweka kwamba kwenye bango, ilikuwa imeandikwa kwamba Tanasha Donna angekuwepo kwa ajili ya kukutana na mashabiki na wala sio kuwatumbuiza.

Also Read
Mamake Diamond afichua babake mzazi

Lakini kwenye maelezo katika mitandao ya kijamii, usimamizi wa sehemu hiyo ya burudani iliongeza kipengee kinachosema kwamba Tanasha angeimba.

Wasimamizi hao waliomba wateja msamaha wakisema Tanasha alikuwa na tatizo kidogo na sauti yake kwa hivyo hangeweza kuimba.

Hii sio mara ya kwanza mwanadada huyo ambaye ana mtoto na Diamond Platnumz wa Tanzania kujipata taabani kwa maswala ya utapeli.

Also Read
Harmonize ashauri wanamuziki chipukizi

Wakati mmoja alizomewa kwenye mitandao ya kijamii kwa kukosa kulipa ada ya huduma alizopata za mapodozi wakati wa kuandaa video ya muziki.

Baadaye tena kuliibuka tetesi kwamba alikosa kulipa ada ya usafiri kwenye teksi.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi