Tanzania kupokea dozi 500,000 aina ya Pfizer kufikia mwisho wa mwezi Oktoba

Jamuhuri ya Tanzania inajizatiti kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Covid-19 huku serikali ya nchi hiyo ikitangaza kuwa inatarajia kupokea  dozi 500,000 za chanjo aina ya Pfizer kufikia mwishoni mwa mwezi Oktoba mwaka 2021.

Akizungumza Jumapili, Oktoba 17, 2021 alipokuwa akitoa taarifa ya wiki ya Serikali jijini Mwanza Msemaji wa Serikali Gerson Msingwa alisema chanjo hizo ni sehemu ya chanjo milioni 1.8 zinazotarajiwa kuletwa nchini Tanzania kupitia mpango wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaolenga kusaidia mapambano dhidi ya vurusi hivyo katika nchi zinazoendelea.

Also Read
COVID-19 Afrika: Wimbi la pili laathiri zaidi kuliko la kwanza
Also Read
Uchaguzi mkuu nchini Iran wavutia Idadi ndogo ya wapiga kura

Kwa mujibu wa Msigwa, hadi kufikia tarehe 15 mwezi Oktoba mwaka 2021, raia 940,000 wa Tanzania, walikuwa wamepokea chanjo aina ya Johnson and Johnson kote nchini humo.

“WHO wanatoa chanjo ili kusaidia angalau asilimia 20 ya watu katika nchi waweze kupatiwa chanjo hizi na hivi karibuni tumepokea chanjo aina ya Sinopharm ambayo kila mtu anatakiwa kuchanjwa mara mbili na zimeshaanza kufika katika kila halmashauri,” amesema Msingwa.

Also Read
Don Jazzy azindua mwanamuziki Ayra Starr

Amewataka wananchi kujitokeza kupatiwa chanjo ya ugonjwa huo ili kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

  

Latest posts

Jeshi la Uganda kusalia DRC hadi litakapotokomeza kundi la ADF

Tom Mathinji

Serikali ya mpito ya Sudan yahimiza kuungwa mkono na Umoja wa Mataifa

Tom Mathinji

FOCAC yanyanyua wakulima wa Afrika kimapato na kuondokana na umasikini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi