Tanzania na Djibouti zafuzu nusu fainali ya CECAFA na kunusia kipute cha AFCON U 17

Tanzania na Djibouti zimejikatia tiketi ya nusu fainali kuwania kombe la Cecafa kwa  chipukizi walio chini ya umri wa miaka 17 nchini  Rwanda , baada ya kutoka sare ya baoa 1-1 katika mechi ya mwisho ya kundi B iliyosakatwa Ijumaa alasiri katika uga wa Umuganda mjini Rubavu.

Abdek Mouhoumed,wa Djibouti alijifunga bao la dakika ya 33 na kuwaweka Serengeti Boys uongozini  kabla ya Moktar Djama Ali kukomboa bao hilo zikisalia dakika 10 mechi ikamilike.
Kufuatia matokeo hayo Tanzania ambao walikuwa wamewabana wenyeji Rwanda magoli 3-1 kwenye mchuano wa ufunguzi wameongoza  kundi hilo kwa pointi 4 huku Djibouti iliyotoka sare na wenyeji ikiibuka ya pili kwa alama 2.
Tanzania  itachuana  na timu ya pili kutoka kundi A katika nusu fainali huku Djibouti ikiweka miadi na viongozi wa kundi A katika semi fainali ya pili  Jumapili kabla ya fainali kusakatwa Disemba 22.
Mataifa mawili bora katika hiyo michuano yatafuzu kuwakilisha ukanda huu katika kipute cha AFCON Juni mwaka ujao nchini Moroko.
  

Latest posts

Emmanuel Korir avunja nuksi na kushinda dhahabu ya kwanza ya Kenya Olimpiki mita 800

Dismas Otuke

Chemutai wa Uganda awaduwaza Wakenya na kunyakua dhahabu ya kwanza ya Olimpiki mita 3000 kuruka viunzi na maji

Dismas Otuke

Sydney McLaughlin avunja rekodi ya dunia ya mita 400 kuruka viunzi wanawake katika Olimpiki

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi