Tanzania wakwea ndege kupiga kipute cha AFCON mwakani

Mabingwa watetezi wa kombe la Cecafa kwa chipukizi walio chini ta umri wa miaka 20 Tanzania wamefuzu kwa kipute cha Afcon mwaka ujao nchini Mauritania, baada ya kuishinda Sudan kusini bao 1-0 katika nusu fainali ya Cecafa iliyopigwa Jumatatu jioni katika uwanja wa Black Rhino Academy kijini Karatu mji wa Arusha Tanzania.

Also Read
Gor Mahia yampiga marufuku katibu mkuu Sam Ochola kwa 'kuuza timu'

Baada ya kipindi cha kwanza kumalizika kwa sare tasa timu zote mbili zilirejea kipindi cha pili kwa lengo la kushinda na kutinga michauno ya Afcon mwakani kwa mara ya  kwanza ,huku kosa la mabeki wa Sudan Kusini kunako dakika ya 58 likimpa fursa Kassim Haruna aliyefunga bao kwa wenyeji maarufu kama Ngorongoro Heroes.

Also Read
Kenya yaanza mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya CECAFA

Licha ya Sudan kujaribu kila mbinu jitihada zao zilizimwa na kuwapa Tanzania tiketi ya kupiga Afcon mwaka ujao  .

Also Read
David Owino Calabar aibwaga manyanga ya Zesco United

Ngorongoro Heroes watashuka dimbani Black Rhino Jumatano hii kuzindua uhasama wa jadi na Uganda Hippos katika fainali ya kombe hilo walilonyakua mwaka jana nchini Uganda.

Sudan Kusini kwa upande wa pili wa sarafu watapambana  na Kenya Jumatano adhuhuri kuwania nafasi ya tatu na nne.

  

Latest posts

Tusker kushikana mashati na Gor Mahia mechi ya kufungua pazia la msimu kuwania kombe la supa

Dismas Otuke

Isabella Mwampambo mkuzaji vipaji vya soka Upendo Friends Sports Academy mjini Arusha Tanzania

Dismas Otuke

Shujaa yashindwa fainali ya kombe kuu na Afrika Kusini 5-38 Vancouver 7’s

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi