Taratibu za upigaji kura wakati wa Uchaguzi Mkuu

Zikiwa zimesalia saa chache kabla ya taifa hili kuandaliwa kwa Uchaguzi Mkuu, ni muhimu zaidi kwa mpiga kura kufahamu na kuzingatia maswala kadhaa katika mchakato wa upigaji kura. 

Umuhimu mkubwa wa kufahamu taratibu za upigaji kura kwanza ni kuhakikisha kuwa kura haziharibiki wala mpiga kura hakosi nafasi ya kumchagua kiongozi anayempenda.

Zingatia yafuatayo siku ya kupiga kura

  1. Beba kitambulisho cha taifa ama pasipoti katika kituo cha kupiga kura, kulingana ulitumia stakabadhi ipi kujisajili kuwa mpiga kura. Kumbuka hutaruhusiwa kupiga kura bila kitambulisho au pasipoti.
  2. Baada ya kutambuliwa na mtambo wa KIEMS, mpiga kura atakabidhiwa karatasi sita za kupiga kura ambazo ni: Karatasi nyeupe ni ya kumchagua Rais, karatasi ya Kijani kumchagua Mbunge, karatasi ya rangi ya biege kumchagua mwakilishi wadi, karatasi ya manjano kumchagua Seneta, karatsi ya zambarau au Purple kumchagua mwakilishi mwanamke na karatasi ya Samawati kumchagua Gavana
  3. Hakikisha karatasi hizo zote, zina muhuri wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC,
  4. Weka alama moja ya kumchagua mwaniaji unayempenda ndani ya sehemu iliyotengwa kwenye karatasi ya kupiga kura.
  5. Kunja karatasi ya kupiga kura huku ukihakikisha alama ya kupiga kura uliyoweka haitasambaa katika eneo lingine.
  6. Weka kila karatasi katika sanduku ya kupiga kura iliyo na kifuniko sawa na rangi ya karatasi.
  7. Kwa wale walio na changamoto ya kusoma na kuandika, au changamoto zingine, andamana na mmoja wa familia yako akusaidie kupiga kura. Anayekusaidia ni sharti abebe kitambulisho chake.
  8. Baada ya kupiga kura, ondoka katika kituo cha kupiga kura.
  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi