TIFA: Uwaniaji Urais wa Raila-Karua ni maarufu zaidi

Utafiti wa hivi punde wa kampuni ya “Trends and Insights For Africa” kwa kifupi -(TIFA), ambao ulifanwya baada ya uteuzi wa wagombea wenza, umeonyesha kwamba Raila sasa anaongoza kwenye kinyang’anyiro cha Urais akiwa na asilimia 39.

Naibu Rais Dkt. William Ruto anachukua nafasi ya pili kwa asilimia 35 huku Kalonzo Musyoka akichukua nafasi ya tatu kwa asilimia 2.

Kulingana na utafiti huo, asilimia 14 ya wale waliohojiwa, walisema bado hawajakata kauli zao, ilhali asilimia moja walisema hawatapiga kura.

Also Read
Serikali kuweka mpaka kati ya mbuga ya Chyulu na shamba la Mikululo

Kuhusu wawaniaji wakuu pamoja na wagombea-wenza wao kwa kutilia maanani swala la jinsia, wanaume wengi wanaegemea upande wa Odinga-Karua na pia Ruto-Gachagua, ijapo idadi ya wanawake waliosema bado hawajakata kauli zao, ni zaidi ya mara mbili ya ile ya wanaume, yaani asilimia 19 na 9 mtawalia.

Kundi la Ruto-Gachagua linafurahia umarufu haswa katika maeneo ya kusini mwa Rift-Valley, Rift-Valley ya kati, maeneo ya mlima Kenya na pia kaskazini mwa Kenya.

Also Read
Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza kuripoti shuleni kuanzia Jumatano

Tiketi ya Musyoka-Sunkuli, ina wafuasi wengi katika maeneo ya Kusini Mashariki mwa nchi, ijapo umaarufu huo wa asilimia 15 hauwezi ukawa wa moja kwa moja.

Kulingana na utafiti huo, muungano wa Raila-Karua unaonekana kuvutia wengi wa wapigaji kura nchini Kenya, Ijapo muungano wa Ruto-Gachagua nao hauko nyuma sana, kwa kutilia maanani umaarufu wao wa asilimia 39 na 35 mtawalia.

Wakati huo huo chama cha UDA ndicho maarufu zaidi kikiwa na asilimia 30, huku chama cha Jubilee kikipoteza umaarufu wake kutoka asilimia 40 hadi tano katika muda wa miezi 16 iliyopita.

Also Read
Kura ya maoni yamweka Naibu Rais William Ruto kifua mbele dhidi ya wawaniaji urais

Chama cha UDA na kile cha  ODM, vina uungwaji mkono wa kitaifa, huku chama cha jubilee na Wiper vikiwa na uungwaji mkono wa maeneo husika, ambapo ni Mlima kenya na eneo la Mashariki mtawalia.

Utafiti huo wa TIFA ulifanywa tarehe 15 hadi 16 mwezi Mei mwaka 2022 kwa kushirikisha watu 1,719.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi