Timu 16 zitakazoshiriki hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika zabainika

Orodha ya timu 16 zilizotinga hatua ya makundi ya kinyang’anyiro cha ligi ya mabingwa Afrika imebainika,kufuatia kukamilika kwa mechi za marudio mchujo wa pili Jumapili usiku.

Kando na miamba 14 waliofuzu kwa hatua ya makundi ya kombe hilo,timu mbili za Juaneng Galaxy ya Botswana na Amazulu Fc kutoka Afrika Kusini ziliandikisha historia kufuzu kwa raundi hiyo kwa mara ya kwanza.

Juaneng licha ya kushindwa mabao 2-0 nyumbani na mabingwa wa Tanzania Simba SC ,walijizatiti na kugeuza matokeo hayo Jumapili jioni walipowazima Simba mabao 3-1 katika mechi ya marudio uwanjani Benjamin Mkapa na limbukeni Juaneng wakafuzu kwa mabao ya ugenini baada ya mechi kuishia sare ya 3-3.

Also Read
Shefield wasajili ushindi wa kwanza ugenini baada ya kuwaduwaza Man U

Amazulu ukipenda Royal Zulu licha ya kushiriki ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza iliwashangaza mabingwa mara tano Toupiza Mazembe ya Drc kwa sheria ya bao la ugenini walipolazimisha sare ya 1-1 mjini Kinsasha kufuatia sare tasa katika duru ya kwanza.

Timu zilizofuzu kwa raundi ya makundi ni mabingwa mara 10 na mabingwa watatezi Al Ahly na mabingwa mara 5 Zamalek wote kutoka Misri,mabingwa mara nne Esperance na mabingwa mara 1 Etoile Du Sahel zote za Tunisia.

Also Read
Harambee Stars watua Agadir tayari kwa mtihani wa Mali
Mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Al Ahly

Algeria itawakilishwa na timu mbili ,washindi mara mbili wa kombe hilo Entete De Setif na CR Belouizdad,wakati Afrika Kusini ikiwakilishwa na mabingwa wa mwaka 2016 Mamelodi Sundowns na Amazulu.

Timu nyingine katika raundi hiyo ya 16 bora ni AC Horoya ambao ni mabingwa wa Guinea,mabingwa wa Angola Sagrada Esperanca Dundo wanaoshiriki kwa mara ya tatu pamoja na wenzao Petro Atletico .

Moroko imetoa timu mbili zilizonyakua kombe hilo mara tano kwa pamoja ikiwa ni Raja Casablanca walioshinda mara tatu na Wydad Casablanca walionyakua kombe hilo mara mbili wakati pia Sudan ikiwa na waakilishi wawili Al Hilal Omdurman na Al Merreikh.

Also Read
Waakilishi wa East Africa waning'inia kubanduliwa CHAN

Washiriki wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi

Misri—Al Ahly,Zamalek
Angola—Petro Atletico,Sagrada Esperanca Dundo
Moroko—Wydad Casablanca,Raja Casablanca
Tunisia–Esperance,Etoile Du Sahel
Sudan—Al Merreikh,Al Hilal Omdurman
Afrika Kusini– Mamelodi Sundowns,Amazulu
Algeria–Entete Setif,CR Belouizdad
Guinea-–AC Horoya
Botswana–-Juaneng Galaxy

Timu 16 zilizoshuka kutoka ligi ya mabingwa zitapangwa na nyingine 16 za kombe la shirikisho kuwania tiketi ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Droo ya makundi ya ligi ya mabingwa inatarajiwa kuandiliwa baadae wiki hii.

  

Latest posts

Dismas Otuke

Omanyala ajiunga na National Police Service

Dismas Otuke

Rais wa zamani wa shirikisho la riadha ulimwenguni IAAF Lamine Diack afariki akiwa na umri wa miaka 88

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi