Timu Kenya ya soka ya watu wenye matatizo ya kuskia yapokea ufadhili wa shilingi milioni 1 kutoka kwa Safaricom

Timu ya soka ya Kenya kwa watu walio na  matatizo ya kuskia  imepokea udhamini wa shilingi milioni 1 kutoka kwa kampuni ya Safaricom .

Ufadhili huo  utagharamia sare za wachezaji na muda wa maongezi kwa timu ya Kenya inayoshiriki mashindano ya soka  yanayoendelea nchini  Kenya  , ya  bara kwa watu walio na matatizo ya kuskia .

Also Read
Idara ya magereza yawatuza washiriki wake wa Olimpiki

Mashindano hayo ambayo  pia yanajumuisha mpira wa kikapu  ni ya kufuzu kwa yale ya dunia ,yanaandaliwa nchini kwa mara ya kwanza tangu yalipoanzishwa mwaka 1924  na yanawaleta pamoja washiriki zaidi ya 1,000 kutoka mataifa 22 ya Afrika .

Also Read
Safaricom kuandaa awamu ya pili ya kikao cha Blaze BYOB Alhamisi usiku

Jumla ya timu 16 za soka na  8 za mpira wa kikapu zinashiriki mashindano hayo katika viwanja vya Kasarani  na Nyayo  na yanatumika kufuzu kwa makala  24 ya mashindano ya dunia kwa watu walio na matatizo ya kuskia  baina ya  Mei 1 na 15 mwaka ujao  mjini  Caxias do Sul, Brazil.

Also Read
Hit Squad yatua Nairobi kutoka Congo ikiwa na medali 13 mkobani

 

  

Latest posts

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi