Timu ya KPA Yakosa Kuingia Fainali

Timu ya voliboli ya KPA ya Kenya ilipoteza nafasi ya kufuzu kwa nusu fainali ya mashindano ya voliboli kati ya vilabu vya bara Afrika kwa wanaume iliposhindwa seti tatu kwa bila na Port Doula ya Cameroon kwenye mechi ya robo fainali.

KPA ilishindwa seti za 17-25, 15-25 na 17-25 na kupoteza fursa ya kutwaa ubingwa wa mwaka huu. Port Doula imefuzu kwa nusu fainali pamoja na Al Ahly ya Misri iliyoilemea Nigeria Customs seti tatu kwa bila za 25-11, 25-16 na 25-9 kwenye mechi ya pili ya robo fainali.

Also Read
Kenya kusubiri zaidi nishani katika Olimpiki ya walemavu Tokyo Japan
Also Read
Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Mashindano hayo ya mwaka huu ya vilabu vya mpira wa Voliboli vya wanaume yalianza rasmi tarehe 8 mwezi huu mjini Kelibia nchini Tunisia. Taifa la Kenya lilikuwa linawakilishwa na timu za Kenya Ports Authority na Equity bank kwenye mashindano hayo.

Timu nyingine za Kenya GSU na Prisons Kenya zilijiondoa kwenye mashindano hayo kufuatia matatizo ya kifedha. Kwenye mashindano ya mwaka jana ya vilabu vya Voliboli barani Afrika nchini Tunisia, KPA ilimaliza katika nafasi ya tano na Equity ilishiriki mashindano hayo kwa mara ya kwanza.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Peter Wahome na Fridah Chepkite washinda Lewa Marathon

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi