Timu ya riadha kuingia kambini wiki hii kujiandaa kwa Olimpiki

Wanariadha 43  waliochaguliwa kuiwakilisha Kenya wanatarajiwa kuripoti kambini katika uwanja wa Kasarani isipokuwa tu wale wa marathon,kujitayarisha kwa makala ya 32 ya michezo ya Olimpiki mjini Tokyo Japan baina ya Julai 23 na Agosti 8.
Kikosi cha Olimpiki
Jumla ya wanariadha 37 walichaguliwa baada ya majaribio ya kitaifa ya siku tatu katika uwanja wa Kasarani kuongezea kwa wale 6 wa marathon ambao waliteuliwa mwaka jana.
Kwa mara ya kwanza Kenya itawakilishwa katika mbio za  mita 100 wanaume  kupitia kwa Fernand Omanyala na Mark Otieno .

Pia wanariadha 30  watakuwa wakishiriki Olimpiki kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja na Ferdinand Omanyala,Mark Otieno, Hellen Syombua,Emmanuel Korir,Moitalel Mpoke,Mary Moraa,Emily Tuwei,Michael Saruni,Emmanuel Korir,Charles Simotwo,Kamar Etyang,Abel Kipsang,Leonard Bett,Abraham Kibiwott,Benjamin Kigen,Nicholas Kimeli,Daniel Simiu,Samuel Chebole,Lilian Kasait,Agnes Tirop,Rodgers Kwemoi,Weldon Langat,Irene Cheptai,Sheila Chelangat,Emily Ngii,Lawrence Cherono,Amos Kipruto,Brigid Kosgei,Ruth Chepngetich na Peres Jepchirchir.
Kati ya wanariadha 43 ,ni 13 pekee watakaokuwa wakirejea Olimpiki  .
Pia majina makubwa yatokosa Olimpiki wakiwemo bingwa wa mita 3000 kuruka viunzi na maji mwaka 2016 Conseslus Kipruto na bingwa wa dunia katika mita 1500 Timothy Cheruiyot.
  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi