Timu za Kenya za Cestoball kutangazwa wakati wa majaribio ya kitaifa kati ya tarehe 13 na 17 mwezi ujao

Shirikisho la mchezo wa Cestoball nchini Kenya , limetangaza kuandaa majaribio ya kitaifa kuteua  timu za taifa za wanaume na wanawake  kati ya tarehe 13 na 17 mwezi  ujao ,katika chuo kikuu cha  Masinde Muliro kaunti ya Kakamega.

Kulingana na Rais wa shirikisho hilo Lawrence Adera jumla ya wachezaji 16 ,wanaume wanane na wanawake wanane  watateuliwa kuelekea Argentina kushiriki mashindano ya kombe la Villa Mercedes Cestoball Cup mjini San Luis baina ya Novemba 22 na Disemba 5  .

Also Read
Azzuri watinga fainali ya Euro baada ya kuwakalifisha Uhispania

“Mashindano haya tutayaandaa katika chuo kikuu cha Masinde Muliro kaunti ya Kakamega  chini ya masharti makali ya Covid 19 ,na ni majaribio ya pili baada ya yale tuliandaa Mombasa maaujuzi katika chuo anuai cha Mombasa TUK” akasema  Adera

Also Read
Abraham Kibiwott na Leonard Bett wafuzu kwa Olimpiki mita 3000 SC ,Bingwa mtetezi Kipruto akosa kumaliza

Timu zilizoshiriki mashindano ya Mombasa mapema mwezi huu kwa wanaume ni  pamoja na Nairobi Eagles,Mathare ,Kenya Prison ,Technical University of Mombasa na Snippers huku timu za akina dada zilizoshiriki zikiwa  Nairobi Stars ,Masinde Muliro University ,Technical University of Mombasa na Mombasa Ladies.

Also Read
Ongare atinga raundi ya pili baada ya kumzaba Mrundi Ornellein mashindano ya Zone 3

Prisons na Masinde Muliro University waliibuka mabingwa katika mashindano hayo ya siku 2 kwa wanaume na wanawake mtawalia.

Cestoball ni mchezo unaochezwa kwa kushirikisha handiboli na  netiboli na hushirikisha wachezaji 6 kila upande na hudumu kwa dakika  40,20 kila kipindi.

  

Latest posts

Omanyala aweka rekodi mpya ya Afrika ya mita 100 ya sekunde 9 nukta 77 Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Wakenya walenga kulipiza cha Olimpiki katika mita 3000 kuruka viunzi na maji katika Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi