Tina Knowles-Lawson amkashifu Piers Morgan

Tina Knowles-Lawson ni mfanyibiashara wa Marekani ambaye anahusika sana na mitindo ya mavazi na ni mamake wanamuziki maarufu Beyonce na Solanje.

Kwenye akaunti yake ya Intagram Tina alipachika video inayomwonyesha Morgan akiondoka kwenye eneo la kutangazia huku akishangaa ni kwa nini hawezi kustahimili kile ambacho yeye mwenyewe alimtendea Megan Markle.

Piers Morgan ni mtangazaji ambaye amekuwa mmoja wa wanaoendesha kipindi kinachofahamika kama “Good Morning Britain” kwenye runinga ya ITV.

Amezungumziwa sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na uamuzi wake wa kumzomea na kumdhalilisha Megan Markle mke wa mwana wa ufalme huko Uingereza Harry baada ya wanandoa hao kufichua kilichosababisha waache kazi katika familia ya Ufalme na kuhamia Marekani.

Siku iliyofuatia, mtangazaji mwenzake Alex Beresford naye alimkosoa Morgan akisema kwamba anaelewa hapendi Morgan lakini hangemchafua namna alivyofanya kwenye kipindi ambacho kinatizamwana watu wengi.

Morgan aliamua kusimama na kuondoka kwenye eneo la kutangazia kipindi hicho kwani hangeweza kustahimili kuzomewa hadharani.

Mama Beyonce anahisi kwamba Morgan anabagua watu wenye asili ya Afrika na ndio maana akaamua kumwonyesha mtangazaji mwenza Alex Beresford. Anashindhwa kuelewa ni kwa nini Morgan anakosa kufikiria mtoto wa Megan na Harry ambaye anaitwa Archie ambaye huenda akaathirika maishani na ubaguzi kama huo.

Baadaye Morgan alirejea kwenye eneo la kutangazia kipindi chao cha “Good Morning Britain” lakini kufikia sasa amejiuzulu baada ya watu zaidi ya elfu 40 kumshtaki kwa ubaguzi na uchunguzi kuanzishwa dhidi yake.

Bila kutaja majina, Megan na Harry kwenye mahojiano yao na mtangazaji Oprah Winfrey walisema kwamba Megan alibaguliwa na kwamba watu wengine kwenye familia ya Harry walikuwa wanahofia mwonekano wa mtoto ambaye walikuwa wakitarajia na tayari uamuzi ulikuwa umefanywa wa kutompa mtoto huyo hadhi ya mwana wa mfalme hata kabla ya kuzaliwa.

Afisi ya Malkia ilijibu madai ya wawili hao kupitia tangazo fupi ambalo lilisema kwamba familia nzima ya ufalme ilisikitishwa na changamoto ambazo Megan na Harry wamepitia kwa muda wa miaka michache iliyopita.

Tangazo hilo lilisema pia kwamba familia itashughulikia madai ibuka kwa faragha na mwisho kusema kwamba Harry, Meghan na Archie wataendelea kuwa watu wanaopendwa kwenye familia hiyo.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi