Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Mwanamuziki wa Canada Tory Lanez kwa jina halisi Daystar Peterson amesababisha minong’ono mitandaoni baada ya kufuta kila kitu kwenye akaunti yake ya Instagram na kupiga kwaheri kwenye akaunti yake ya Twitter. Kwenye twitter aliandika “It’s been real”.

Jamaa huyo amekuwa akizungumziwa sana kutokana na kisa ambapo alimfyatulia risasi mwanamuziki Megan Thee Stallion na kumjeruhi kwenye mguu ambacho kilisababisha Megan amshtaki.

Also Read
Kajala hana akili hata robo! adai Mange Kimambi

Lanez hata hivyo alitumia muziki kwenye albamu yake ambayo inaitwa “Daystar” kukanusha madai ya Megan na kumrejelea kama mwongo. Wengi hawajui kilichosababisha Tory Lanez agure mitandao ya kijamii lakini inadhaniwa kwamba mwanamuziki huyo amefungwa jela.

Megan na Lanez walikuwa wapenzi na mwezi Julai mwaka 2020 walihudhuria sherehe nyumbani kwa kylie Jenner ambapo mvutano ulitokea kati yao na milio ya risasi ikasikika. Megan alipachika picha kwenye mitandao ya kijamii baadaye akionyesha kisigino kilichoshonwa akidai kwamba alipigwa risasi na Lanez.

Also Read
Travis Scott aletea binti yake wa miaka 3 Basi ya shule

Afisi ya wakili katika wilaya ya Los Angeles ndiyo iliweka kesi hiyo mahakamani na alipofikishwa mahakamani mwezi Novemba mwaka 2020, Tory Lanez alikana mashtaka dhidi yake. Hapo ndipo mahakama iliamuru kwamba asizungumzie kesi hiyo kabisa.

Also Read
Bobi Wine aangaziwa kwenye Spotify

Mwezi Januari mwaka huu wa 2021, Lanez aliweka ombi mbele ya mahakama la kuruhusiwa kuzungumza kuhusu kesi dhidi yake kwani Megan alikuwa akiizungumzia.

  

Latest posts

Arrow Bwoy Amefiwa

Marion Bosire

Shona Ferguson Ashinda Tuzo Hata Baada Ya Kifo

Marion Bosire

Snoop Dogg Atangaza Kifo Cha Mamake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi