Trevor Noah Atangaza Kifo cha Nyanyake

Mchekeshaji wa asili ya Afrika Kusini ambaye sasa anaishi na kufanya kazi Marekani ametangaza kifo cha nyanyake mpendwa. Alipachika kwenye mitandao ya kijamii, video ya kumbukumbu inayomwonyesha akicheka na nyanyake ambaye alikuwa anafahamika kama Frances Noah ambaye anasikika akimuuliza atatabasamu vipi bila meno mdomoni.

Kulingana na tangazo la Trevor ambaye huongoza kipindi cha “The Daily Show”, Gogo (kama alivyopenda kumrejelea) alizikwa jana Alhamisi asubuhi. Anamsifia akisema alikuwa na kumbukumbu sawa hata ingawa alikuwa amezeeka sana. Frances aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 95 na alikuwa na uhusiano wa karibu sana na Trevor maanake alimlea baada ya mamake Trevor ambaye ni binti ya Frances kuolewa.

Also Read
P Funk Majani abadili kazi

“Leo asubuhi familia yangu ilizika mmoja wetu mkongwe zaidi Frances Noah, au Gogo jinsi wengi walimrejelea. Nyanyangu alizaliwa mwaka 1927 na hata kama alikuwa na umri wa miaka 95, alikuwa na kumbukumbu nzuri kutuhusu sote. Kila wakati nilikaa naye nilihisi ni kama ni safari ya kipekee kwani alikumbuka nyakati zote nzuri za familia, nyakati za huzuni na hata mafanikio.

Nyumba yake huko Soweto haikuwa nyumba tu, ilikuwa kimbilio la wanawake wengine ambao hawakua na pa kwenda, mahali ambapo watu wa jamii wangekusanyika kuomba kila wiki, mahali ambapo kila mmoja alihakikishiwa upendo.

Also Read
Siku ya Kimataifa ya Busu

Najua wengi mlimpenda Gogo kutoka mbali na ninashukuru kwa jumbe ambazo mmetuma. Nimelia wiki nzima nikisherehekea filamu ya kipekee ambayo nimewahi kutizama. Simulizi lilioanza wakati nilipumua kwa mara ya kwanza kabisa na kukamilika na pumzi yake ya mwisho. Mwanamke aliyenionyesha mapenzi ya kweli. Aliaga akiwa amelala na hata akatubariki na sherehe moja ya mwisho ya siku ya kina mama ulimwenguni ambayo alifurahia sana.” ndiyo maneno ya Trevor kwenye mitandao ya kijamii.

Mchekeshaji huyo alifanya umma umfahamu nyanyake wakati alimzuru nyumbani kwake huko Soweto, Afrika kusini ambapo ziara yake humo na mazungumzo yao yalinakiliwa kwa video ambayo aliisambaza mitandaoni. Alimkumbusha jinsi alikuwa mtoto mtundu ambaye alitaka kila mara kucheza na watoto wengine barabarani huku nyanyake akijua kweli alikuwa katika hatari kubwa ya kuchukuliwa na maafisa wa polisi wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini.

Also Read
Trevor Noah Azomea Wanaobagua Mwigizaji wa Asili ya Afrika

Kulingana na Gogo wakati huo watu weusi hawakuwa wanaruhusiwa kujumuika na wazungu na Trevor ambaye babake mzazi ni mzungu angetwaliwa. Gogo alisema kwenye hiyo video kwamba alilazimika kumchapa Trevor kila mara kama njia ya kumkanya asitoke nje.

  

Latest posts

Harusi ya Nandy Kuwa ya Awamu Tatu

Marion Bosire

Mwigizaji Mkongwe wa Nollywood Kenneth Aguba Apata Usaidizi

Marion Bosire

Travis Baker Arejea Kazini

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi