Trump aondoka katika Ikulu ya Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump ameondoka katika Ikulu ya Marekani akiwa ameandamana na mkewe Melania Trump saa chache kabla ya kuapishwa kwa Rais mteule Joe Biden.

Rais huyo na mkewe walielekea katika kambi ya kijeshi iliyoko Maryland ambapo sherehe za mwisho za kuwaaga zilipangiwa kuandaliwa.

Also Read
Hongera wanawake wa Afrika Mashariki, lakini kuna ya kujifunza kutoka kwa wanawake wa China

Hata hivyo makamu wa Rais, Mike Pence hatahudhuria sherehe za kumuaga Trump lakini anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Biden na Harris baadae Jumatano.

Rais Trump akiwahutubia wafuasi wake aliwatakia mafanikio Rais mteule Joe Biden na makamu wake Kamala Harris licha ya kuwa hakuwataja wawili hao kwa majina.

Also Read
Joe Biden ahimiza utulivu msimu wa baridi unapoghubika Marekani

Alisema akiwa katika ikulu ya Marekani aliafikia mengi licha ya janga la Covid-19 kuathiri kipindi cha miezi tisa iliyopita cha utawala wake

Vifo vilivyotokana na Covid-19 nchini humo sasa ni zaidi ya 400,000, na idadi ya vifo imeendelea kuongezeka.

Also Read
Bara la Afrika lasifiwa kwa kudhibiti Covid-19

Rais Mteule Joe Biden na makamu wake Kamala Harris wanatarajiwa kuapishwa baadaye Jumatano katika hafla itakayoongozwa na jaji mkuu John Roberts.

Sherehe ya kuapishwa kwa Biden itahudhuriwa na marais wa zamani Barack Obama,Bill Clinton na George W Bush.

Biden atakuwa rais wa Marekani wa 46.

  

Latest posts

Babu wa Loliondo aliyepata umaarufu wa kutibu magonjwa sugu amefariki

Tom Mathinji

Israeli: Iran ilishambulia Meli ya kubeba mafuta katika Pwani ya Oman

Tom Mathinji

Australia kuwatumia wanajeshi kutekeleza masharti dhidi ya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi