Trump asema anapata nafuu ila changamoto zaidi ni siku chache zijazo

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaendelea kupata afueni ya kiafya ila siku chache zijazo ndizo zitakazokuwa na changamoto halisi kufuatia kuambukizwa kwakwe virusi vya Corona.

Trump amesema hayo kupitia ukanda wa video aliyotuma katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter akiwa hospitalini anakotibiwa ugonjwa wa COVID-19 kwa siku ya pili sasa.

Jumamosi, daktari wa rais huyo alisema kuwa Trump amepiga hatua kubwa za afueni ila bado hajakuwa huru kabisa kutokana na hatari ya ugonjwa huo.

Also Read
Visa 291 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Siku hiyo ilikumbwa na taarifa kinzani kuhusiana na hali ya kiafya ya Rais Trump.

Muda mfupi baada ya kikosi cha wahudumu wa afya kutoa taarifa hiyo ya afueni, Mkuu wa Wafanyikazi wa Ikulu Mark Meadows alitoa taarifa nyengine na kusema hali ya Trump ni ya kutia wasiwasi sana.

Also Read
Ni vizuri maabara zote zinazoshukiwa kuwa chanzo cha COVID-19 zichunguzwe

Wandani wa Rais Trump wanasema kuwa hakupendezwa na maneno ya Meadows.

Watu kadhaa waliokuwa karibu na rais huyo pia wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona akiwemo mkewe Melania Trump.

Wengi kati yao walihudhuria hafla ya watu wengi Ikulu juma lililopita kuhusu uteuzi wa Coney Barrett kama Jaji wa Mahakama ya Juu Zaidi na inaaminika kuwa hafla hiyo ndiyo iliyosababisha ueneaji wa virusi hivyo kwa kasi.

Also Read
Huenda jumuiya ya ECOWAS ikaiondolea Mali vikwazo

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Marekani, msaidizi wa karibu wa Trump Nicholas Luna ndiye wa hivi karibuni kuambukizwa ugonjwa hio.

Kuambukizwa COVID-19 kwa Trump kunaonekana kulemaza shughuli zake za kampeni ya kutaka kuchaguliwa tena kama rais wa Marekani.

Trump atakabiliana na mpinzani wake Joe Biden katika uchaguzi huo utakaofanyika tarehe tatu mwezi ujao.

  

Latest posts

Kiongozi wa kijeshi nchini Burkina Faso Henri Damiba atimuliwa

Tom Mathinji

Mkuu wa Junta Burkina Faso atoa wito wa utulivu nchini humo

Tom Mathinji

Maadhimisho ya miaka 73 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi