Tume ya EACC na shirika la KBC zashirikiana katika vita dhidi ya ufisadi

Tume ya maadili na kupambana na ufisadi hapa nchini EACC na shirika la utangazaji nchini KBC, zimeshirikiana katika vita dhidi ya ufisadi kupitia utoaji mafunzo kwa wasimamizi wakuu wa KBC.

Mafunzo hayo yanawalenga mameneja 16 ambao watakuwa wanachama wa Kamati ya kuzuia ufisadi katika shirika la KBC.

Tume ya IEBC ilifadhili warsha iliyoandaliwa kwa njia ya video kuhusu ufisadi na utovu wa maadili iliyoandaliwa siku ya Jumatano.

Also Read
Wajane wa Murunga waitaka mahakama iwaruhusu wamzike mume wao

Mafunzo hayo yatawapa mameneja hao ujuzi wa kuzuia visa vya ufisadi katika maeneo yao ya kazi.

Afisa mkuu Mtendaji wa EACC Twalib Mbarak, katika hotuba yake ya ufunguzi iliyosomwa kwa niaba yake na naibu mkurugenzi  Gilbert Lukhoba, alitoa wito kwa mameneja hao kuwa mabalozi wa kuleta mabadiliko kwa kuhakikisha maadili mema katika taasisi yao kwa kufuata sheria, masharti, sera na miongozo ya maafisa wa umma.

Also Read
Wamiliki timbo zinazohatarisha maisha kaunti ya Nakuru kushtakiwa

Mbarak aliwakumbusha mameneja hao kuwa ufanisi au kufeli kwa vita dhidi ya ufisadi hapa nchini, hakutegemei EACC, lakini kunategemea jinsi vyombo vya habari vitakavyokumbatia maadili katika utendakazi wao.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji humu nchini KBC, Dkt. Naim Bilal, alisema mafunzo hayo yanakusudi kuimarisha jukumu la ukaguzi la shirika la KBC.

Also Read
Ujio mpya wa Darubini michezo

Dkt. Bilal alisema lengo lake ni kuona kuwa shirika la KBC linaendeshwa kwa njia iliyo wazi na yenye uwajibikaji.

Kamati ya kuzuia ufisadi ilibuniwa kwa lengo la kukabiliana na ufisadi katika utumishi wa umma.

Taasisi za Umma zinahitajika kubuni Kamati za kukabiliana na ufisadi Kulingana na mwongozo uliotolewa wa utendakazi.

  

Latest posts

Rais Kenyatta amwomboleza Nancy Karoney, dadake waziri wa ardhi Farida Karoney

Tom Mathinji

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi