Tume ya usawa na jinsia yataka sheria kupitishwa kukabiliana na dhuluma za kijinsia

Tume ya taifa kuhusu usawa na jinsia imehimiza kupitishwa kwa sheria za kukabiliana na dhuluma za kijinsia katika kila kaunti.

Mwenyekiti wa tume hiyo Dkt. Joyce Mwikali Mutinda amesema wasichana wengi walikuwa waathiriwa wa dhuluma za kimapenzi na wakawa wajaa wazito baada ya shule kufungwa kwa muda mrefu mwaka uliopita kufuatia janga la COVID-19.

Also Read
Wanafunzi 68 wa shule ya upili ya wasichana ya Bahati waambukizwa Covid-19

‚ÄúSitaki kuzungumza kuhusu wazazi peke yao, kuna watu wengi waliowadhulumu wasichana na kuwatunga mimba kwa sababu hakuna sheria inayowalinda,” alisema Mwikali.

Also Read
Guinea yaondolewa katika Jumuiya ya ECOWAS

Alitoa wito kwa serikali ya taifa kupitia kwa bunge kupitisha mswada kuwahusu watoto.

Dkt. Mutinda aliwapongza wazee kutoka jamii ya Samburu kwa kutangaza kukomeshwa ukeketaji wasichana wakisema haki zai sharti zilindwe.

Dkt. Mutinda alisema haya mjini Maralal katika kaunti ya Samburu wakati wa warsha kuhusu usawa wa kijinsia.

Also Read
Watu 24 wafariki kutokana na makali ya Covid-19 huku visa 1,344 vipya vikinakiliwa nchini

Vijana waliohudhuria warsha hiyo walisema wametengwa kwenye maendeleo wakihimiza serikali kuhakikisha ugavi na utumizi sawa wa rasilimali miongoni mwa makundi yenye mahitaji maalum.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi