Tusker Fc na Gor Mahia huenda walazimike kucheza mechi za Afrika katika nchi jirani

Miamba wa soka nchini Gor Mahia na mabingwa watetezi wa ligi kuu Tusker Fc huenda wakalazimika kucheza mechi zao ya kombe la shirikisho msimu huu katika nchini jirani baada ya shirikisho la kandanda Afrika , kutangaza kuwa uwanja wa kitaifa wa Nyayo na ule wa kimataifa wa Kasarani havikidhi viwango vinavyohitajika kuandaa mechi hizo.

Also Read
Stars yaendeleza mazoezi kujiandaa kukabiliana na Misri na Togo

Kwa mjibu wa barua ya CAF iliyoandikiwa FKFK tarehe 17 mwezi huu ,baada ya kukamilika kwa mechi za sasa za kufuzu kombe la dunia mwaka ujao Kenya ikiwa na mchuano mmoja nyumbani dhidi ya Rwanda mwezi ujao,hakuna mechi yoyote ya kimataifa itakayoandaliwa katika uwanja wa Nyayo na Kasarani hadi pale marekebisho mwafaka yaliyopendekezwa yatekelezwe.

Also Read
Mulee ana imani Kenya kuwashinda Misri na Togo
Tusker wakichuana na Zamalek Sc uwanjani Nyayo

Kamati ya CAF ya ukaguzi wa viwanja ilikuwa imepiga marufuku matumizi ya uwanja wa kimataifa wa Kasarani na kuidhinisha ule wa Nyayo pekee kwa michuano ya kimataifa .

Tusker Fc wameratibiwa kuchuana na CS Sfaxien ya Tunisia huku Gor Mahia ikiwaandaa AS Otoho d’Oyo ya Congobaina ya Novemba 28 na December 4 katika raundi ya mwisho ya mchujo kuwania kombe la shirikisho Afrika.

Also Read
Samuel Gathimba kuongoza timu ya Kenya kwa mashindano ya dunia ya Race Walking nchini Oman

Upo uwezekano mkubwa wa waakilishi wa Kenya Gor na Tusker kuwaalika wapinzani wao katika taifa jirani kufuatia uamuzi huo.

Kulingana na ripoti ya CAF uwanja wa Nyayo hauna taa za kutosha na pia hauna eneo na wanahabari .

  

Latest posts

Boro wamtimua meneja Chris Wilder kwa matokeo duni

Dismas Otuke

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi