Tusker FC wabanwa koo na Wazito na kuyumbisha harakati za kuwahi tiketi ya Ligi ya mabingwa

Vinara wa ligi kuu nchini Tusker Fc waliendelea kuyumbayumba katika mechi ya pili mtawalia walipolazimishwa kutoka sara ya bao 1 katika mchuano pekee uliopigwa Ijumaa alasiri katika uwanja wa Utalii jijini Nairobi.

Beki Sammy Mejja aliwaweka wageni Tusker uongozini kwa bao la dakika ya nne ya mchezo kabla ya  Kevin Kimani kusawazishia wenyeji katika dakika ya 21 na pambano kumalizika kwa sare.

Also Read
Homeboyz wazidiwa Uzito ligi kuu FKF

Kufuatia matokeo hayo Tusker wangali kushikili kukutu uongozi wa ligi hiyo kwa alama 35, baada ya mechi 17 wakifuatwa na  KCB kwa pointi 33  wakati AFC Leopards ikiwa ya tatu kwa alama 32.

Also Read
Yehualew avunja rekodi ya dunia marathon iliyoandikishwa na Ruth Chepngetich April mwaka huu

Ligi hiyo itaendelea Jumamosi kwa  michuano minne,Ulinzi Stars wakifungua dimba dhidi ya Kariobangi Sharks saa saba uwnajani Narok  wakati Westrern Stima ikiwa mwenyeji wa   Kakamega Homeboyz uwanjani Bukhungu .

Also Read
Mkufunzi wa makipa wa Gor Mahia Willis Ochieng ajiuzulu

Posta Rangers watakuwa Kasarani dhidi ya Afc Leopards wakati Nzoia Sugar ikiwa nyumbani Sudi dhidi ya Mathare United.

  

Latest posts

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

FKF yakatiza mkataba wa shilingi milioni 127 na Odibets

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi