Tusker Fc wameilemea Gor Mahia magoli 8-7 kupitia mikiki ya penati Jumatano adhuhuri na kunyakua kombe la FKF Super ,katika mechi ngumu iliyopigwa katika kiwara cha manispaa ya Thika.
Gor walichukua uongozi wa dakika ya 54 kupitia kwa bao la Samuel Onyango kwa njia ya penati kufuatia kipa wa Tusker Brian Bwire kumchezea ngware mshambulizi Benson Omalla .
Wagema mvinyo Tusker walirejea mchezoni dakika 2 baadae kwa bao lake Ibrahim Joshua pia kupitia mkwaju wa penati kufuatia , Boniface Muchiri pia kuangushwa kwenye eneo la D.
Pambano hilo lilikatika kwa sare ya bao 1-1 baada ya dakika 90 huku kipa wa Tusker Brian Bwire akiibeba Tusker alipopangua mkwaju wa penati wake Ernest Wendo naye Kalos Kirenge akaunganisha penati ya mwisho ya Tusker na kupata ushindi wa 8-7.
Msimu wa mwaka 2021/2022 wa ligi kuu ya Kenya utang’oa nanga Jumamosi hii ambapo Tusker watakuwa wakitetea taji.