Mabingwa watetezi Tusker FC,Gor Mahia na AFC Leopards wamesajili sare katika mechi za ligi kuu zilizochezwa Jumapili.

Sofapaka ikicheza ugenini katika uwanja wa Ruaraka ,ililazimisha sare tasa dhidi ya wenyeji Tusker Fc wakati Gor Mahia pia ikiambulia sare ya bila kwa bila dhidi ya Bandari FC uchanjaa wa kitaifa wa Nyayo,huku AFC Leopards wa wakipoteza uongozi na kwenda sare ya 1-1 na Vihiga Bullets waliopandishwa ngazi ligini msimu huu.

Katika michuano mengine iliyopigwa Jumapili,mashambulizi Derrick Otenga na kiungo Michael Oduor wakipachika bao 1 kila mmoja katika ushindi wa KCB wa 2-0 dhidi ya wanajeshi Ulinzi Stars.

Posta Rangers pia waliikomoa Talanta FC mabao mawili bila jawabu.
Gor ,KCB na Homeboyz wanaongoza jedwali kwa pointi 18 kila moja , baada ya mechi 9 za msimu huu.