Tusker kushikana mashati na Gor Mahia mechi ya kufungua pazia la msimu kuwania kombe la supa

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Kenya Tusker Fc watashuka katika uwanja wa manispaa ya Thika kumenyana na mabingwa wa kombe la FKF Gor Mahia katika pambano la kufungua pazia la msimu wa ligi kuu nchini unaotrajiwa kung’oa nanga mwishoni mwa juma hili.

Also Read
Mashabiki hawataruhisiwa uwanjani Kasarani mechi ya Kenya na Misri

Mchuano huo utaanza saa saba adhuhuri na kwa desturi ndio utakuwa wa kuashiria msimu mpya ,pande zote zikiwindataji ya kwanza.

Tusker watacheza mechi hiyo wakiwa roho juu baada ya kufuzu kwa mchujo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi washindi mara nne wa taji hiyo Zamalek kutoka Misri.

Also Read
Mulee awajumuisha limbukeni katika kikosi cha Harambee Stars kwa mechi za kufuzu AFCON

Tusker waliiparakasa timu ya Arta Sola 7 ya Djibouti mabao 3-0 Jumamosi iliyopita katika uwanja wa Nyayo na kuingia raundi ifuatayo kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-1.

Also Read
Gor Mahia watoka nyuma na kuicharanga Merowe 3-1

Gor hajakua na matayarisho kabambe wakicheza tu mechi za kujipiga msasa.

Msimu mpya wa mwaka 2021/2022 wa ligi kuu utaanza Jumamosi hii Septemba 25 Tusker FC wakianza kutetea taji dhidi ya AFC Leopards huku Gor wakianza msimu dhidi ya KCB.

  

Latest posts

Tusker waleweshwa nyumbani na Zamalek 1-0

Dismas Otuke

Tysa yasherekea miaka 20 ya kubadilisha vijana Kitale kupitia soka

Dismas Otuke

Ni Siku ya Ndovu kumla mwanawe Tusker dhidi ya Zamalek Nyayo

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi