Tusker yailewesha Rangers wakati Sharks wakikosa heshima ugenini Mumias

Wagema mvinyo Tusker Fc wamewaka hai ya kunyakua taji ya 12 ya ligi kuu ya Kenya na ya kwanza tangu mwaka 2016 baada ya kuinyofoa Posta Rangers magoli 4-1 katika mchuano wa ligi hiyo uliopigwa Alhamisi Alasiri katika uwanja wa  kimataifa wa Kasarani.

John Macharia  aliwaweka wenyeji Tusker  uongozini kwa bao la dakika ya 38 ,kabla ya Ezekiel Okware kuisawazishia Rangers dakika moja baadae, huku  John Meja akiwaweka tena wana mvinyo uongozini kwa bao la pili katika dakika ya pili ya nyongeza kipindi cha kwanza.

Also Read
Faith Kipyegon asajili muda wa nne wa kasi duniani katika mita 1500

Katika kipindi cha pili Tusker waliendeleza mashambulizi na kudhihirisha mchezo mzuri huku wakiongeza bao la tatu dakika ya  67 kupitia kwa Luke Namanda kabla ya Mejja kupiga jingine  dakika ya 84.

Also Read
Ingwe yapigwa na stima huku Tusker wakikatwa makali na Mathare

Ushindi huo umehahikisha Tusker wanaendelea kushikilia kukutu uongozi wa jedwali la ligi hiyo kwa pointi 29 kutokana na mechi 12 ,wakishinda 9 kwenda sare 2 na kupoteza mmoja wakifuatwa na Kenya Commercial Bank kwa alama 25 ingawa  vinara hao wa ligi wakiwa wamecheza mechi 2 zaidi.

Katika mkwangurano mwingine Kariobangi Sharks wamekwea hadi nafasi ya tatu ligini kufuatia ushindi wa bao 1 kwa bila ugenini dhidi Vihiga United uwanjani Mumias Complex Erick Kapaito akipachika bao la pekee na la ushindi  katika dakika ya 79 .

Also Read
Tusker Fc yanusia ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya 12 ,baada ya kuwaangusha Kakamega Homeboyz

Bao hilo limehakikisha Kapaito anaendelea kuongoza msimamo wa ufungaji magoli akiwa amebusu nyavu mara 13 huku ushindi huo ukiwaweka Sharks kwa alama 21.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi