Tuzo za kukuza mauzo zaanzishwa Uganda

Serikali ya Uganda imeanzisha tuzo za mitindo ya mavazi na mabango kwa lengo la kukuza biashara nchini humo chini ya kauli mbiu ya “BUBU” yaani “Buy Uganda Build Uganda”.

Waziri wa biashara nchini humo Harriet Ntabazi alisema tuzo hizo ambazo zitakuwa zikifanyika kila mwaka zinalenga kuonyesha jukumu walilo nalo wasanii na watu wengine katika sekta ya burudani la kuhimiza matumizi ya bidhaa zilizoundwa nchini humo.

Also Read
Maafisa wa usalama nchini Uganda washtumiwa kwa kuwajeruhi wanahabari waliokuwa wakiripoti kumhusu Bobi Wine

Awamu ya mwaka huu ya tuzo hizo itaandaliwa tarehe 17 mwezi Disemba mwaka 2021.

“Wadau wa sekta ya burudani kama vile wanamuziki, wacheza densi, wachekeshaji na waigizaji wana mchango mkubwa katika kukuza hulka ya watu kupenda bidhaa mbali mbali ulimwenguni. Nasi tumeonelea itakuwa njia mwafaka kutumia wasanii wetu kama mabalozi wa bidhaa zetu.” Alisema waziri Harriet Ntabazi wakati wa kuzindua rasmi tuzo hizo.

Also Read
Wawili wauawa kwenye shambulizi la bomu Kampala

Wizara ya biashara nchini Uganda itaweka kando wiki nzima kwa ajili ya maonyesho ya bidhaa mbali mbali katika sehemu tofauti nchini humo. Bidhaa zitakazoonyeshwa ni pamoja na mavazi, bidhaa za ngozi kati ya nyingine nyingi ili wizara hiyo itambue sehemu ambayo itaongeza fedha zaidi ili bidhaa hizo ziundwe kwa wingi na kuuzwa kimataifa.

Kiongozi wa chama cha wachekeshaji nchini Uganda Hannington Bugingo alikaribisha tuzo hizo akisisitiza lengo ni kuwafanya wasanii mabalozi wa bidhaa za Uganda huku mwenyekiti wa chama cha wanamuziki Isaac Rucci akisema sekta ya muziki ni kiungo muhimu ambacho kinatumiwa na kampuni tofauti kusukuma bidhaa sokoni.

Also Read
Msitumie madhabahu kubagua mashoga - Kirk Franklin

Mwanzilishi wa kampuni ya Soko Uganda ambayo huhimiza watu kununua bidhaa za Uganda Hillary Mbabazi naye alielezea kwamba walielekeza juhudi zao kwa wasanii kwani wanatambua uwezo mkubwa walionao.

  

Latest posts

Yul Edochie Amsifu Babake

Marion Bosire

Aki Na Paw Paw Warejea

Marion Bosire

Harmonize Atoa Orodha Ya Nyimbo Za Albamu Mpya

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi