Mwaniaji Urais wa shirikisho la soka nchini FKF Twaha Mbarak ,ameahidi kuzilipia klabu zote za wanawake ada ya kushiriki, illi kuafikia makataa ya kujisali ifikiapo Februari 24.
Akizungumza Jumatatu baada ya kukutana na waakilishi wa timu 9 zinazoshiriki ligi kuu ya wanawake ,katika ya Nakuru , Mbarak amesisitiza kuhakikisha timu hizo zinatimiza masharti yaliyowekwa na kamati ya muda ya FKF ya kupendekeza vlabu vyote kujisajili kabla ya tarehe 24 mwezi huu.

“Ili kufuata masharti yote na kuhakikisha timu zote za wanawake zinaruhusiwa kushiriki kwenye zoezi la kupiga kura baade mwaka huu ,ni vyema tujisajili kwa mjibu wa FKF caretaker comittee”
“Kama hatua ya kwanza ni kuhakisha hamna timu inafungiwa nje ya upigaji kura “akaongeza Twaha
Mwakilishi wa timu hizo Beryl Oketch alitoa hakikisho la kumuunga Twaha akimtaja kuwa suluhisho kwa changamoto nyiNgi zinazokumba soka yetu ya Kenya ,haswa katika kuinua soka ya wanawake.
Kwenye ziara hiyo Twaha alitoa mchango wa mipira miwili ya soka kwa kila klabu ya ligi kuu ya wanawake pamoja na sare za kuchezea mechi za ligi kuu.
Timu hizo pia kwa kauli moja zimelaani hatua ya aliyekuwa katibu mkuu wa FKF Barry Otieno kufuatia hatua yake ya kuandika barua kwa Caf kujiondoa kwa Kenya kwa mechi za kufuzu kwa kombe
bara Afrika dhidi ya Crested Cranes ya Uganda.
Kikao hicho kilihudhuriwa na timu za Gaspo Women, Nakuru City Queens, Kangemi Ladies, Kayole Starlets, Thika Queens,Bunyore Starlets, Vihiga Queens, Wadadia na Kisumu All Starlets huku Zetech FC, Uinzi Starlets FC na Trans Nzoia Falcons zikituma udhuru.
Twaha ametangaza kuwa anapania kuzuru kaunti zote 47 nchini , kuzungumza na waakilishi wa timu zinazoshiriki ligi kuu KPL,NSL, na Division one, ili kuzisaidia kutimisha masharti ya usajili ifikiapo makataa ya tarehe 24 mwezi huu.
Twaha ametangaza kuwania Urais wa FKF na mwaniaji mwenza Andrew Amukoa ,huku kamati ya muda ikitarajiwa kutangaza mikakati ya na mpangilio kuelekea uchaguzi huo.