Twaha Mbarak ameahidi kurejesha hadhi ya soka ya Kenya

Mwaniaji Urais wa shirikisho la kandanda Kenya FKF ,Twaha Mbarak ameahidi kurejesha hadhi ya soka ya Kenya endapo atachaguliwa kinara kwenye uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa mwaka huu.

Kwenye mahojiano na KBC ,Mbarak ambaye ni mchezaji wa zamani amesema kuwa baadhi ya mambo atakayoyapa kipa umbele endapo atapewa jukumu la uongozi wa kandanda  ni pamoja na:kubuni chama cha akiba na mikopo kwa wachezaji wa ligi kuu,kuianisha muungano mmoja wa wachezaji wastaafu,kuleta usawa wa uteuzi wa wachezaji katika timu ya Harambee Stars,kuanzisha mpangilio bora wa soka ya chipukizi,na kuimarisha kandanda ya wanawake.

Also Read
Tusker kushikana mashati na Gor Mahia mechi ya kufungua pazia la msimu kuwania kombe la supa
Twaha Mbarak kwenye picha na wachezaji wastaafu katika uwanja wa City

“Endapo nitafanikiwa kutwaa uongozi wa FKF,nitawaweka pamoja wachezaji wastaafu katika  chama kimoja,na kuwaweka katika sacco wachezaji wa ligi kuu  ili wakistaafu wawe angaa na kitu cha kuwasaidia,pia nataka kuweka mpangilio bora na mahususi wa soka nchini  ile Youth Structure  ambapo kutakuwa na timu za chipukizi za kutoa wachezaji kwa timu za taifa ,kuleta usawa wa uteuzi wachezaji kwenye timu ya taifa Harambee Stars  na kulainisha na kuimarisha soka ya wanawake”akasema Mbarak

Also Read
Agnes Tirop aweka rekodi mpya ya dunia ya kilomita 10 ya dakika 30 na sekunde 1 katika
Twaha akitoa hundi ya shilingi laki mbili kwa timu ya wachezaji wastaafu

Mbarak ambaye alikuwa amewania Urais katika uchaguzi uliopita   bila mafanikio,  alikuwa akizungumza haya siku ya Jumatano katika uwanja wa City alipowazuru wachezaji wastaafu wa Kenya kwenye mazoezi na kuwapa shilingi laki mbili za kugharamia usafiri wao kwenda Uganda kwa mechi za kujipima nguvu.

Also Read
Kenya kuandaa makala ya kwanza ya CECAFA women Champions League

Mbarak atakuwa akiwania Uenyekiti wa FKF kwa ushirikiano na  Andrew Amukoa atakayekuwa naibu wake kwenye uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa ufikiapo April mwaka huu na kamati ya muda iliyoteuliwa na waziri Amina kundesha soka ,baada ya kuvunjilia mbali FKF iliyokuwa ikiongozwa na Nick Mwendwa.

 

  

Latest posts

Riadha Kenya kuandaa seminaa kwa wanariadha Januari 21 kutangulia mashindano ya kitaifa

Dismas Otuke

Polisi wachunguza mauaji ya mwanamke aliyepatikana ndani ya sanduku

Tom Mathinji

Kenya haitatuma timu kwa michezo ya Olimpiki ya majira ya Baridi Beijing

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi