Uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Matungu kuandaliwa mwezi Machi 2021

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza kwamba uchaguzi mdogo wa Eneo Bunge la Matungu utafanyika tarehe nne mwezi Machi, mwaka wa 2021.

Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati ametangaza hatua hiyo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi, aliyetangaza kiti hicho cha ubunge kuwa wazi.

Also Read
Jopo labuniwa kutatua changamoto katika mbuga ya kitaifa ya Nairobi

Kwenye taarifa rasmi ya gazeti lililochapishwa Jumanne, Chebukati ameongeza kuwa chaguzi ndogo za wadi mbali mbali pia zitaandaliwa siku hiyo.

Wadi hizo ni pamoja na Huruma iliyoko Kaunti ya Uasin Gishu, Hells Gate na London zilizoko Kaunti ya Nakuru, Kiamokama iliyoko Kaunti ya Kisii na Kitise/Kithuku katika Kaunti ya Makueni.

Also Read
Wapenzi wa BBI kuanza kukusanya saini milioni moja wiki hii

IEBC imewahimiza wale wenye nia ya kugombea viti hivyo kudumisha kanuni za kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19 kwenye mchakato mzima wa chaguzi hizo ndogo.

Also Read
IEBC yakanusha kuwa mifumo yake imedukuliwa

Kiti cha ubunge katika eneo la Matungu kiliachwa wazi baada ya kifo cha aliyekuwa Mbunge Justus Murunga Makokha.

Murunga alifariki mnamo tarehe 14 mwezi Novemba, wakati alipokuwa akipelekwa hospitalini huko Mumias, Kaunti ya Kakamega.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi