Uchaguzi mkuu nchini Iran wavutia Idadi ndogo ya wapiga kura

Wapiga kura nchini Iran wanajiandaa kupiga kura zao Ijumaa kwenye uchaguzi wa urais,ambao huenda kiongozi wa kidini Ebrahim Raisi akashinda.

Baada ya kampeini ambazo hazijawavutia watu wengi,idadi ya wapiga kura inatarajiwa kuwa ya chini katika nchi hiyo ambayo uchumi wake umelemazwa na vikwazo vya kiuchumi vya Marekani na janga la Covid-19.

Also Read
Afisa mkuu wa zamani wa kituo cha polisi cha Mukuyani atozwa faini ya 200,000 kwa kupokea hongo

Kiongozi mkuu wa kidini wa taifa hilo Ayatolla Ali Khamenei alipiga kura yake mapema Ijumaa asubuhi kwenye msikiti mmoja karibu na afisi zake katika mji mkuu wa nchi hiyo Teheran.

Also Read
Israeli yaonya kuhusu ufaafu wa Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raisi

Upigaji kura utatamatishwa usiku wa manane,huku matokeo yakitarajiwa Jumamosi.

Mshindi wa uchaguzi huo ataapishwa kuwa Rais wa nane wa taifa hilo na atachukua wadhifa wa uongozi kutoka kwa Rais Hassan Rouhani,mwenye siasa za wastani ambaye amehudumu kwa vipindi viwili vya miaka minne kila kimoja ,jinsi ilivyoratibiwa kwenye katiba ya taifa hilo.

Also Read
Iran yataka Umoja wa Mataifa kulaani mauaji ya Mohsen Fakhri-Zadeh

Mamlaka makuu ya utawala tangu mapinduzi ya mwaka 1979 yamo mikononi mwa kiongozi mkuu wa kidini wa taifa hilo Ayatolla Ali Khamenei.

  

Latest posts

Jeshi la Uganda kusalia DRC hadi litakapotokomeza kundi la ADF

Tom Mathinji

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi