Uchaguzi wa Kiambaa sio taswira ya uchaguzi mkuu ujao asema Dkt Matsanga

Chama kipya cha UDA  kinachohusishwa na naibu Rais William Ruto kilipata ushindi katika uchaguzi mdogo wa kiambaa wiki iliyopita kupitia kwa mgombezi wake John Njuguna Wanjiku aliyepata asilimia 50   huku  mgombezi wa chama tawala  cha Jubilee  Kariri Njama akiibuka wa pili kwa asilimia 49.

Kwa mjibu wa mchanganuzi wa siasa Dkt David Matsanga uchaguzi huo mdogo haukuwa vita baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake ,baada ya Rais kukosa kumfanyia kampeini mgombezi wa chake kinyume na alivyofanya Ruto,hivyo haipaswi kuchukuliwa kuwa Rais amepoteza umaarufu eneo la mkoa wa kati .

Also Read
Sharlet Mariam ajitoa kwenye uchaguzi mdogo wa Msambweni

“Rais Uhuru ni kiongozi wa kitaifa bali si wa kabila na yeye kukosa kumfanyia kampeini mgombezi wa chama chake ilikuwa jambo la busara,matokeo ya uchaguzi huo hayamaanishi kuwa Rais amepoteza uungwaji mkono katika ngome yake”

Also Read
Millie Odhiambo: Marekebisho ya Kikatiba hayatadhoofisha bunge la Senate

“Hii pia haitoi taswira  yoyote kwa uchaguzi wa mwaka ujao  hivyo wanachama na viongozi wa vyama vyote Jubilee na UDA wanapaswa kutengeza sera bora na mikakati mwafaka ” akasema Matsanga

Matsanga pia amemkosoa Naibu Rais Ruto akisema kuwa  mvutano uliopo kati ya Jubillee na UDA hauna manufaa yoyote kwa taifa.

Also Read
Idadi jumla ya maambukizi ya Covid-19 hapa nchini sasa imefika 96,458

“Inasikitisha sana kuona kuwa naibu Rais angali anapinga Jubilee akiwa ndani ya serikali,ingekuwa busara kama angejiondoa serkalini na aanze kujenga chake akijiandaa kwa uchaguzi wa mwaka ujao” akaongeza Matsanga

Wafuasi wa Jubilee na wale wa chama cha UDA wamekuwa wakifarakana hadharani  kuashiria mianya na sintofahamu nyingi  huku kila kimoja kikijaribu kudhihirisha ubabe.

  

Latest posts

Vifo vya ndugu wawili vyazua taharuki Embu Kaskazini

Tom Mathinji

Gladys Erude ameaga dunia

Marion Bosire

Wavuvi wapata mabomu sita katika Ziwa Victoria

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi