Uchaguzi wa Ugavana kaunti ya Mombasa na Kakamega umeahirishwa

Uchaguzi wa Ugavana uliokuwa umepangwa kuandaliwa tarehe 23 mwezi Agosti katika kaunti ya Mombasa na Kakamega, umeahirishwa.

Tume huru ya Uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC kupitia kwa taarifa, imesema hatua hiyo imetokana na vitisho na dhuluma dhidhi ya maafisa wa tume hiyo katika ukumbi wa Bomas, ambao  bado hawajafika afisini wakihofia maisha yao.

“Vitisho hivyo vimewahofisha maafisa wa ambao wameshindwa kuripoti kazini. Unyanyasaji huo sharti usitishwe,” alisema mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Also Read
Sakaja kuzindua Manifesto yake Alhamisi usiku

Vurumai zilizoshuhudiwa katika ukumbi wa Bomas wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais, zilisababisha kujeruhiwa kwa baadhi ya makamishna wa tume hiyo wakiwemo, Abdi Guliye, Boya Molu na afisa mkuu mtendaji Marjan Marjan.

Chebukati pia ameahirisha uchaguzi wa maeneo-bunge ya Kitui Rural,kaunti ya Kitui, Kacheliba na Pokot Kusini katika kaunti ya Pokot Magharibi,likiwemo eneo-bunge la Rongai,katika kaunti ya Nakuru.

Also Read
Rais Kenyatta aonya dhidi ya kueneza uwongo kuhusu chanjo ya Covid-19

Maeneo mengine ambapo uchaguzi huo umeahirishwa ni pamoja na wadi ya Nyaki Magharibi,katika eneo-bunge la Imenti kaskazini,kaunti ya Meru, Kwa Njenga, katika eneo-bunge la Embakasi Kusini,kaunti ya Nairobi.

Wakati uo huo,Chebukati ametuma risala za rambirambi kwa familia ya mwendazake,afisa mkuu wa IEBC eneo bunge la Embakasi Mashariki Daniel Musyoka aliyepatikana akiwa ameuawa.

Also Read
Ni walio na cheti cha COVID-19 ndio watahudumiwa katika afisi za kaunti ya Kakamega

Anasema tume hiyo ilipigwa na butwaa kutokana na mauaji ya Musyoka ambaye mwili wake ulipatikana ukiwa umetupwa msituni katika eneo la Loitoktok,kaunti ya Kajiado.

Mwenyekiti huyo wa IEBC amezitaka asasi za usalama kuharakisha uchunguzi wao na kuwatia mbaroni waliomuua Musyoka.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi