Na Ripota Wetu.
Treni za abiria katika jiji la Nairobi zitarejelea shughuli zao Jumatatu baada ya kusimamisha shughuli zao kwa wiki moja.
Shirika la reli hapa nchini mnamo tarehe 26 mwezi Disemba lilisimamisha shughuli za treni hizo jijini Nairobi na kutumia mabasi yake kuwasafirisha abiria hadi Nanyuki baada ya nafasi za treni hizo kuuzwa.
Vituo vikuu vya kusimama kwa mabasi ya shirika hilo yanayotumia barabara za Westlands ni Jeevanjee, Museum Hill, CFC Stanbic, Chiromo, kituo cha mabasi cha Westlands, Brookside, Safaricom, ABSA, ABC Place, na James Gichuru.
Kwenye barabara ya Upper Hill , mabasi hayo yatachukua na kushukisha abiria katika vituo vya Meladin, KMA, CIC, Britam, TSC, Kadhis Court, CBC, KASNEB, na kituo cha hospitali ya kitaifa ya Kenyatta KNH.
Kwenye barabara ya Yaya Centre mabasi hayo yatachukua na kushukisha abiria katika vituo vya Serena, Integrity Centre, Chancery, Maktaba Kuu, Nairobi Hospital, D.O.D, Hurlingham, Chaka Place, na Yaya Centre.
Wakati huo huo abiria kutoka eneo la Eastland na maeneo ya Kaskazini ya jiji kwa mara nyingine watafurahia huduma za reli zilizokuwa zimesimamishwa kuanzia tarehe 18 mwezi Disemba.