Uchukuzi wa umma watakiwa kuzingatia masharti ya kudhibiti Covid-19

Waziri wa Uchukuzi James Macharia ametoa wito kwa wakenya wanaotumia uchukuzi wa umma wazingatie kikamilifu kanuni za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa COVID-19.

Aidha waziri huyo aliwataka wahudumu wa uchukuzi wa umma vile vile watekeleze mikakati iliyowekwa ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

Also Read
Wanasiasa watakiwa kutowagawanya wakenya wakati wa msimu wa Uchaguzi

Kulingana na waziri huyo wa uchukuzi, kanuni kuhusu ugonjwa wa Covid -19 zingalipo na zinapaswa kutekeleza ipasavyo ili kuendelea kutoa huduma za uchukuzi wa watu na bidhaa na vile vile kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.

Also Read
Vijana katika kaunti ya Machakos wahimizwa kujihusisha na shughuli za kiuchumi

Alisema lengo la kuangamiza ugonjwa wa COVID-19 litaafikiwa, wadau wote wakishirikiana na kutekeleza wajibu wao wa kibinafsi na wa pamoja.

Agizo hilo la Waziri huyo wa uchukuzi linajiri baada ya serikali kuongeza muda wa kutekelezwa kwa kafyu kote nchini kwa lengo la kudhibiti msambao wa Covid19.

Also Read
Watu 10 zaidi wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Siku ya Ijumaa, serikali pia ilipiga marufuku mikusanyiko yote ya umma,ikiwemo mikutano ya afisini.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi