UDA haitaandaa Uteuzi katika eneo bunge la Kamukunji na Embakasi Mashariki

Chama cha  United Democratic Alliance (UDA), hakitaandaa uteuzi katika maeneo bunge ya Kamukunji na Embakasi Mashariki. 

Badala yake, chama hicho kitatumia njia mbadala zinazokubaliwa na katiba ya chama, kuwateua wawaniaji wake.

Also Read
Chama Cha UDA Chaandaa Uteuzi Kiambaa

Mwenyekiti wa kitaifa wa bodi ya uchaguzi Anthony Mwaura, alisema hakutakuwa na uteuzi wa pamoja kati ya chama cha UDA na kile cha Amani National Congress party (ANC), katika maeneo bunge ya Dagoreti Kaskazini na  Mathare, akisema mbinu mbadala zitatumika kuwatambua wawaniaji.

Also Read
Mudavadi atoa wito wa mdahalo wa kitaifa kuhusu mswada wa BBI

“Hatua hii inamaanisha kuwa hakutakuwa na shughuli za uteuzi miongoni mwa vyama tanzu jinsi ilivyotangazwa hapo awali,” alisema Mwaura.

Also Read
Chama cha UDA kumtangaza William Ruto kuwa mgombeaji wake wa kiti cha Urais

Wakati huo huo, shughuli ya uteuzi wa wawaniaji wa ubunge na wadi zote katika eneo bunge la Roysambu katika kaunti ya Nairobi, itaendelea tarehe 20 mwezi Aprili jinsi ilivyopangwa.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi