UDA yakaribisha maombi kwa wanaotaka kuwania nyadhifa tatu za MCA

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimekaribisha maombi kwa wale wanaotaka kuwania  nyadhifa tatu za uwakilishi wadi katika chaguzi ndogo zijazo.

Mwaliko huo unajiri kabla ya kuandaliwa kwa chaguzi ndogo tatu tarehe 14 mwezi Octoba mwaka 2021, katika wadi za Eldas kaunti ya Wajir, wadi ya Kiagu kaunti ya Meru na wadi ya Nguu/ Masumbaini katika kaunti ya Makueni.

Also Read
Watu 528 waambukizwa Covid-19 nchini huku watu wanne wakifariki

Mwaniaji wa kiti cha mwakilishi wadi atahitajika kulipa shilingi 30,000 huku wawaniaji  wadhifa wa wawakilishi wa vijana, wanawake na walio na ulemavu, watalipa shilingi 20,000.

Kupitia kwa ilani, katibu mkuu wa chama cha UDA Veronica Maina, aliwahimiza wawaniaji waliohitimu kutuma maombi yao kwa chaguzi hizo tatu kufikia kabla tarehe 4 mwezi Agosti mwaka 2021 saa sita adhuhuri, katika makao makuu ya chama hicho kilichoko katika jumba la Hustlers, lililoko barabara ya  Makindi Jijini Nairobi.

Also Read
Rashid Echesa apuuza agizo la kujisalimisha kwa Polisi

Vile vile Maina aliongeza kuwa maombi hayo yanaweza tumwa kupitia kwa tovuti ya UDA.

Kiti cha uwakilishi wadi cha Eldas kilibaki wazi baada ya Ibrahim Abass, kuaga dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Also Read
Polisi wanachunguza mauaji ya kikatili ya mwanahabari wa shirika la KBC

Kiti cha uwakilishi wadi cha  Kiagu kilibaki wazi baada ya Eunice Karegi kufariki kutokana na Saratani huku Nguu/Masumba kilisalia baada ya Harrison Ngui kufariki kupitia ajali ya barabarani katika barabara kuu ya Mombasa-Nairobi.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi