Ufaransa na Poland zarejesha masharti ya kudhibiti Covid-19

Ufaransa na Poland zimerejesha masharti ya kuzuia msambao wa ugonjwa wa Covid-19 huku nchi hizo zikinakili ongezeko kubwa katika maambukizi mapya.

Takriban watu millioni 21 wanatarajiwa kuathirika na hatua hiyo.

Nchini Poland migahawa,vituo vya kitamaduni na viwanja vya michezo vitafungwa kwa majuma matatu.

Also Read
Angela Merkel ashinikiza kufungwa kwa shughuli nchini Ujerumani kudhibiti Covid-19

Hayo yanajiri huku nchi hiyo pia ikinakili ongezeko kubwa zaidi katika maambukizi ya kila siku tangu mwezi Novemba mwaka uliopita.

Also Read
Kenya yapokea zaidi ya dozi 400,000 za chanjo ya Astrazeneca kutoka Uingereza

Visa vya maambukizi mapya pia vimeripotiwa kuongezeka nchini Ujerumani huku Chansela Angela Merkel akionya kuwa huenda nchi hiyo ikarejesha marufuku ya usafiri,miongoni mwa masharti mengine.

Utoaji wa chanjo katika baadhi ya mataifa ya muungano wa Ulaya umetatizwa na ucheleweshaji wa usambazaji wa chanjo.

Also Read
Afueni kwa Trump baada ya Bunge la Seneti kupungukiwa na kura za kumshitaki

Mataifa mengine barani humo pia yalikuwa yamesimamisha matumizi ya chanjo ya Oxford-AstraZeneca kufwatia hofu kuhusiana na madhara yake.

  

Latest posts

Shule nchini Uganda kufunguliwa Januari mwaka 2022

Tom Mathinji

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi