Ufaransa yafunga shule kwa wiki tatu kudhibiti msambao wa Covid-19

Rais  Emmanuel Macron  wa  Ufaransa amesema shule nchini humo  zitafungwa kwa muda wa wiki tatu kama sehemu ya hatua mpya za kitaifa  za   kupambana na  visa vinavyoongezeka vya maradhi ya  Covid.

Macron alisema kuwa shule zitaendesha  na  masomo   kwa njia ya mtandao  kuanzia wiki ijayo.

Katika hotuba kwa taifa kupitia runinga Jumatano usiku, Macron alisema kuwa juhudi zaidi zinahitajika kukabiliana na janga na Covid-19 ambalo linazidi kuongezeka.

Hatua za kuzuia usafiri zilizotangazwa  katika maeneo kadhaa ya Ufaransa mapema mwezi huu, pia zitahusisha   maeneo zaidi.

Duka zote ambazo sio hazuizi bidhaa muhimu  zitafungwa kuanzia  Jumamosi na kutakuwa na marufuku ya watu  kusafiri zaidi ya Kilometa 10 kutoka nyumbani  kwao bila sababu ya msingi.

Rais huyo alisema shughuli ya utoaji wa chanjo inapaswa kuharakishwa huku taifa hilo likiashiria kuwa ni asilimia 12 ya watu nchini humo ambao wamechanjwa dhidi ya Covid-19.

Nchi hiyo ina zaidi ya watu 5,000 ambao wamelazwa katika wadi za wagonjwa mahututi hospitalini. Mnamo  Jumatano, wizara ya afya  iliripoti visa vipya 59,038.

Ufaransa hadi sasa imeripoti zaidi ya visa milioni 4.6 vya maambukizi ya maradhi ya Covid-19 na 95,495 vifo vinavyohusiana na maradhi hayo.

  

Latest posts

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdock wakamatwa na kupelekwa mafichoni

Dismas Otuke

Vikosi vya usalama vyazima jaribio la mapinduzi nchini Sudan

Tom Mathinji

China yaadhimisha miaka 50 tangu kurudishiwa kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi