Ufaransa yaweka marufuku ya usafiri katika mji mkuu wa Paris

Mji Mkuu wa Ufaransa, Paris, umepangiwa kuanza kudumisha marufuku ya usafiri ya mwezi mmoja, ili kukabiliana na maradhi ya COVID-19, huku nchi hiyo ikihofia kuzuka kwa wimbi la tatu la maambukizi hayo.

Maeneo mengine 15 nchini humo pia yatadumisha masharti hayo kuanzia leo usiku wa manane.

Hata hivyo hatua hizo zimelegezwa kuliko ilivyokuwa awali, huku watu wakiruhusiwa kufanya mazoezi ya nje.

Chini ya hatua hizo mpya, biashara ambazo sio muhimu zitafungwa, ingawa shule zitaendelea na shughuli zake.

Watu hawataruhusiwa kusafiri kwenda sehemu zingine za nchi, isipokuwa wale walio na sababu muhimu.

Ufaransa imethibitisha zaidi ya visa vipya elfu 35 katika masaa 24 yaliyopita. Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Jean Castex alisema kuna uwezekano mkubwa wa kutokea wimbi la tatu la maambukizi nchini humo.

Mjini Paris, watu 1,200 wako katika wadi za wagonjwa mahututi, idadi ambayo ni kubwa kuliko ilivyokuwa katika kilele cha wimbi la pili la maambukizi mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita.

 

  

Latest posts

Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdock wakamatwa na kupelekwa mafichoni

Dismas Otuke

Vikosi vya usalama vyazima jaribio la mapinduzi nchini Sudan

Tom Mathinji

China yaadhimisha miaka 50 tangu kurudishiwa kiti chake kwenye Umoja wa Mataifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi