Uganda Cranes watua Nairobi tayari kukabiliana na Harambee Stars Septemba 2

Timu ya taifa ya Uganda Cranes imetua jijini Nairobi Jumatatu usiku tayari kwa mpambano wa kwanza wa kundi E , kufuzu kwa fainali za kombe la dunia dhidi ya wenyeji Harambee Stars ya Kenya Septemba 2 katika uwanja wa taifa wa Nyayo.

Also Read
Michezo ya Olimpiki haitaahirishwa kamwe 2021 asema Bach

Kikosi cha Uganda kikiongozwa na kocha mkuu Milutin Sredejovic kiliwasili katika angatua ya kimataifa ya Jomokenyatta mida ya saa tano na robo Jumatatu usiku .

Also Read
Taharuki ya kiusalama yatanda nchini Uganda kabla uchaguzi mkuu Alhamisi
Kocha wa Uganda Milutin Mitcho

Uganda watachuana na Kenya Alhamisi saa tisa alasiri katika uga wa taifa wa Nyayo ikiwa mechi ya kwanza ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Qatar.

Also Read
FC Talanta yavishwa taji ya NSL huku Vihiga Bullets ikipandishwa hadi ligi kuu FKF kwa mara ya kwanza

Baadae Kenya watazuru Rwanda kumenyana na wenyeji Amavubi Septemba 5 wakati Uganda wakiwa nyumbani dhidi ya Mali uwanjani Namboole.

Harambee Stars wakipiga mazoezi

Timu itakayoongoza kundi hilo itafuzu kwa raundi ya mchujo na ya mwisho.

  

Latest posts

Sala asaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Liverpool

Dismas Otuke

Pambano la Kenya na DRC kuwinda tiketi ya kombe la dunia katika kikapu laahirishwa

Dismas Otuke

Msimu wa nne wa raga Dala 7’s kuanza Jumamosi

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi