Uganda Hippos yalenga kombe la kwanza huku Ghana wakiwania kombe la 4 AFCON U 20

Fainali ya makala ya 16 kuwania kombe la mataifa ya Afrika kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20 itasakatwa Jumamosi usiku katika uwanja wa Olympic mjini Nouakchott Mauritania baina ya mabingwa mara tatu Ghana maarufu kama black sateolites dhidi ya Uganda Hippos wanaoshiriki kwa mara ya kwanza.

Also Read
Harambee Stars yapanda nafasi mbili msimamo wa FIFA

Ghana wanawinda kombe la kwanza baada ya miaka 12 iliyopita .

 

Uganda iliibuka ya pili kutoka kundi A kwa kupata ushindi dhidi ya Msumbiji na Mauritania kabla ya kuibandua Burkina Faso kupitia penati katika robo fainali na baade kuinyuka Tunisia magoli 4-1 katika nusu fainali.

Also Read
Ahly kuivaa Berkane fainali ya 29 ya kombe la CAF Supa live kupitia KBC Channel 1

Ghana iliibuka ya tatu katika kundi lao ikiwashinda Tanzania na kwenda sare na Moroko, huku wakiibandua Cameroon katika kwota fainali kupitia mikiki ya penati na hatimaye kuitema Gambia bao 1-0 kwenye nusu fainali.

Also Read
Gor Mahia tayari kuwashika mateka wanajeshi APR Jumamosi

Ghana itawategemea mfungaji wao bora Percious Boah,Abdul Fatawu na mshambulizi Emmanuel Agyemang Duah huku Uganda ikihitaji uwajibikaji kutoka kwa nahodha Gvain Kizito,mfungaji bora Derrick Kakooza na Richard Basangwa .

  

Latest posts

Faith Kipyegon kufunga msimu nyumbani Kip Keino Classic

Dismas Otuke

Gatlin na Omanyala tayari kuonyesha ubora wao Kip Keino Classic Jumamosi

Dismas Otuke

FKF yakosolewa kwa kumtimua kocha Jacob Mulee wakati usiofaa

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi