Uganda na Tanzania zafuzu AFCON U 17 mwakani nchini Moroko

Uganda na Tanzania zimefuzu kwa kipute cha kombe la AFCON mwezi Juni mwaka ujao nchini Moroko, baada ya kujikatia tiketi kwa nusu fainali za kombe la CECAFA nchini Rwanda siku ya Jumapili.

Also Read
Super Unfair! Babu Tale azomewa na mwanawe.

Uganda walihitaji bao lake Oscar Mawa kuwabandua  Djibouti katika nusu fainali ya kwanza uwanjani Umuganda wilayani Rubavu, huku Tanzania maarufu kama Serengeti boys wakiishinda Ethiopia penati 4-3  kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Also Read
Mwamuzi wa Kenya Kamaku kusimamia mechi ya Nigeria dhidi ya Sierra Leone

Ni mara ya pili mtawalia  kwa timu za Uganda na Tanzania kufuzu kwa kipute cha AFCON kwa chipukizi baada ya timu zao kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 20 kufuzu maajuzi nchini Tanzania.

Also Read
Luis Enrique kuzawadiwa kandarasi mpya kuinoa Uhispania punde wakifuzu kwa kombe la dunia

Fainali ya Jumanne ya Cecafa itatanguliwa na mchuano wa kuwania nafasi ya tatu na nne kati ya Ethiopia na Djibouti katika uga wa Umuganda.

  

Latest posts

Elain Thompson awaongoza vidosho wa Jamaica kufagia medali zote za mita 100

Dismas Otuke

Kenya yaambulia pakavu baada ya Moraa kukosa kufuzu kwa fainali ya ita 800 vipusa

Dismas Otuke

Omanyala Omurwa afuzu kwa nusu fainali ya mita 100 Olimpiki na kusawazisha rekodi ya kitaifa

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi