Uganda yaipakata Kenya 5-0 na kutinga nusu fainali CECAFA U 17

Mabingwa watetezi Uganda wamefuzu kwa nusu fainali ya michuano ya kombe la CECAFA kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17  nchini Rwanda baada ya kuigaragaza Kenya mabao 5-0 katika mechi ya mwisho ya kundi A  iliyopigwa Jumatano adhuhuri uwanjani Umuganda mjini Rubavu .

Oscar Mawa  aliwaweka Uganda maarufu kama Cubs kifua mbele kwa bao la dakika ya 7 lililodumu hadi mapumzikoni.

Waganda waliondelea kucheza mchezo wa kuonana vyema kunako kipindi cha pili huku safu ya ulinzi ya Kenya ikionekana kuishiwa nguvu nao washambulizi wakikosa makali  na ilichukua dakika 9 pekee kabla ya Mawa kuongeza mabao mawili ya haraka dakika ya 50 na 54 na kukamilisha Hat trick yake katika mchezo huo.

Also Read
Ni kufa kupona kwa Kenya Pipeline na Kenya Prisons nchini Tunisia Jumatatu

Travis Mutyaba na Ronald Madoi waliongeza goli moja kila mmoja katika dakika za 78 na 88 na kudidimiza matumaini ya Kenya kufuzu kwa nusu fainali kwani itawalazimu Ethiopia ambao pia wamo kundi A na Kenya ,wapoteze kwa mabao 6-0  katika mchuano wa Ijumaa dhidi ya uganda  ili Kenya inayofunzwa na kocha  Oliver Page  ifuzu nusu fainali.

Also Read
Gor Mahia yamsajili chipukizi Jules Ulimwengu
Timu ya Uganda kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 17

Kenya ni ya mwisho katika kundi A kwa alama 1 baada ya kukamilisha mechi zake kufuatia kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Ethiopia  katika pambano la ufunguzi Jumapili iliyopita .

Timu ya Kenya kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 17

Uganda waliocheza mechi moja wanaongoza kundi hilo kwa alama 3 na wanahitaji tu sare dhidi ya Ethiopia katika mechi ya mwisho ili kumaliza ya kwanza.

Also Read
CAF yakubali ombi la Gor na kuahirisha mechi ya ligi ya mabingwa hadi Jumamosi

Tanzania ilikuwa ya kwanza kufuzu kwa nusu fainali kutoka kundi B  siku ya Jumanne  baada ya kuwazabua wenyeji Rwanda mabao 3-1.

Michuano hiyo ya Cecafa itaingia hatua ya nusu fainali tarehe 20 nayo fainali isakatwe Disemba 22 ambapo mataifa mawili bora yatafuzu kucheza fainali za kombe la AFCON kwa vijana wasiozidi umri wa miaka  17 mwezi Juni mwaka ujao nchini Moroko.

 

  

Latest posts

Emmanuel Korir avunja nuksi na kushinda dhahabu ya kwanza ya Kenya Olimpiki mita 800

Dismas Otuke

Chemutai wa Uganda awaduwaza Wakenya na kunyakua dhahabu ya kwanza ya Olimpiki mita 3000 kuruka viunzi na maji

Dismas Otuke

Sydney McLaughlin avunja rekodi ya dunia ya mita 400 kuruka viunzi wanawake katika Olimpiki

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi