Uhaba mkubwa wa maji Garissa huenda ukasababisha kufungwa kwa shule na hospitali

Shule na hospitali katika kaunti ya Garissa zimo katika hatari ya kufungwa kwa sababu ya ukosefu wa maji.

Akizungumza katika mji wa Garissa, mwakilishi wa  wa wadi ya  Modogashe, Ali Gure,  alisema hali ni mbaya katika Kaunti Ndogo ya Lagdera ambapo maelfu ya watu wanahitaji chakula cha msaada.

Also Read
Familia kadhaa kutoka sehemu kame kunufaika na ufadhili wa miaka mitatu

Alisema wamekuwa wakitegemea malori ya maji kusambaza maji kwa wakaazi lakini hayatoshi kuwahudumia maelfu ya wakaazi ambao sasa wanahitaji bidhaa hiyo.

Gure alisema changamoto za usalama katika mipaka ya Lagdera na Isiolo zinaweza kuzidishwa zaidi na ukosefu wa maji ya kutosha na malisho kwa wanyama wakati watu wanapigania visima vichache vya maji katika eneo hilo.

Also Read
Wito watolewa wa uchunguzi kufanywa kuhusu miili iliyopatikana Mto Tana

Viongozi hao wametoa wito kwa  serikali ya  Kitaifa na wafadhili kusaidia kupunguza athari za ukame, na haswa ukosefu wa maji katika kaunti hiyo.

Also Read
Kituo cha utafiti wa ugonjwa wa Saratani chazinduliwa hapa nchini

Kaunti ya Garissa kama kaunti jirani katika eneo la  Kaskazini Mashariki, imepokea  mvua  ya kiwango cha cini na kwa sababu hiyo,  mabwawa  mengi  madogo madogo ya  kukusanya  maji   hayakukusanya maji ya kutosha  na   hakuna  nyasi ya  kutosha kwenye  maeneo ya malisho.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi